Friday, 22 December 2017
Wanachama wa UN watupilia mbali vitisho vya Trump
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekaidi vitisho vya Serikali ya Marekani na kupiga kura ya ndiyo kuidhinisha azimio linalotupilia mbali tangazo la Rais Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel.
Nchi wanachama 128 zilipiga kura ya ndiyo dhidi ya kura tisa zilizopinga, huku nchi 35 zikijiondoa kupiga kura.
Baada ya kura, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley aliyashukuru mataifa 65 yaliyopinga azimio hilo, yaliyojizuia kupiga kura au hayakuwapo wakati wa kupiga kura.
Marekani, Togo, Honduras na Guatemala ni mataifa ambayo yalipiga kura kupinga azimio hilo.
Mataifa ya Canada, Mexico, Rwanda, Uganda, Poland, Jamhuri ya Czech na Romania hayakupiga kura.
Kabla ya kura, Marekani ilitishia kuzuia misaada kwa mataifa yatakayopiga kura kuunga mkono azimio hilo.
Haley amesema kura hiyo haitabadilisha kitu katika mipango ya Marekani kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem kutoka Tel Aviv.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment