Uzinduzi wa barabara ya kuingia katika Hospitali ya CCBRT
Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta amezindua ujenzi wa barabara ya CCBRT
kwa kiwango cha Lami, ambapo imekuwa mbovu kwa muda mrefu hali ambayo
iliyopelekea kuleta shida kwa wakazi na madereva waliokuwa wakiitumia
barabara hiyo.
Akizungumza leo hii mara baada ya kufanya uzinduzi huo, Meya Sitta
amesema barabara hiyo ni miongoni mwa barabara muhimu katika manispaa ya
kinondoni ,ambapo pia hutumika kwa wagonjwa wengi kuingia katika
Hospitali ya CCBRT iliyopo Msasani eneo la Macho Jijini Dar es salaam.
Sitta ameeleza kuwa barabara hiyo imekuwa kero kubwa ,hivyo waandishi
wa habari walikuwa wakimulika eneo hilo mara kwa mara ,na kubainisha
kuwa tayari barabara hiyo imeshapatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake Meneja Mradi wa barabara hiyo Bw.Abdallah Yasin Msemo,
amesema barabara hiyo itakamilika ifikapo tarehe 14-3-2018.
Ameongeza kuwa tatizo kubwa ambalo lilikuwa likiikumba barabara hiyo ni
maji ambayo yalikuwa yakituama na kukosa eneo la kwenda,hivyo katika
ujenzi huo utaambatana na mitaro itakayowekwa pembeni ya barabara hiyo
ili kusaidia maji kupita panastahili.
No comments:
Post a Comment