Friday, 8 December 2017

Rais wa zamani wa Argentina kukamatwa

Cristina Fernández de Kirchner aliwashauri watu wa Argentina kutetea sheria
Jaji nchini Argentina anataka rais wa zamani wa nchi hiyo Cristina Fernández de Kirchner akamatwe kwa madai kuwa alitumia siasa kujikinga.
Bi Fernandez ambaye aliongoza kwa miaka minane kutoka Disemba mwaka 2007, alichaguliwa hivi majuzi kuwa seneta na hivyo ana kinga ya bunge.
Ili apate kukamatwa, bunge na Senate litahitaji kuondoa kinga hiyo kwa njia ya kura.
Ameitaja hatua hiyo kama upuzi ambayo inakiuka sheria.
Maseneta walisema kwa watalitathmini ombi hilo la jaji wakati watalipokea.
Jaji Claudio Bonadio, ambaye anatakja rais huyo wa zamani akamatwe anasema kuwa Bi Fernandez alishiriki katika mpango wa kufukina kuhusika kwa maafisa wa vyeo vya juu wa Iran mwaka 1994 wakati wa shambulizi la bomu kwenye kituo cha kiyahudi mjini Buenos Aires.

Jaji Bonadio pia aliamrisha Héctor Timerman, ambaye alikuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni chini ya Bi Fernández kuwekwa kizuizi cha nyumbani kufuatia na kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment