Kirusi hicho kilidaiwa kuvamia zaidi ya kampuni 300,000 kwenye mataifa 150 na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola.
Thomas Bossert ambaye ni msadizi wa Rais Donald Trump, aliyasema haya kupitia jarida la Wall Street Journal, Hii ndiyo mara ya kwanza Marekani imeilaumu Korea Kaskazimni kwa kirusi hicho.
Bw. Bossert anayemshauri Trump katika masuala ya usalama wa ndani wa nchi alisema kuwa madai hayo ni kutokana na ushahidi uliopo.
Serikali ya Uingereza na kampuni ya kompiuta ya Microsof waliilaumu Korea Kaskazini kwa kirusi hicho.
Mwezi Mei kompiuta zinazotumia Windows zilivamiwa na kirusi hicho na kufungwa ambapo watumiaji walitakiwa kulipa ili kuweza kupata data zao.
No comments:
Post a Comment