Chanzo cha fujo hiyo kinatajwa kwamba ni kitendo cha Manchester City kushangilia sana na kupiga kelele nyingi, jambo hilo liliwakera baadhi ya watu wa United akiwemo Jose Mourinho na mvutano ulianzia hapo.
Pep Gurdiola ambaye ndiye aliwaongoza vijana wake kuichapa United bao 2 kwa 1 amesema hawakuwa na nia ya kuwakera Manchester United kwani wao walikuwa wakishangilia tu lakini kama wamekereka anawaomba msamaha.
“Lakini na wao kuna michezo ambayo walishinda na wakashangilia sana, sisi tumeshinda Derby na tulipaswa kufurahia hilo na kama limewaudhi tunaomba radhi kwa kila mtu wa United aliyekereka” alisema Pep.
Pep Gurdiola amesisitiza kwamba akama timu ikifanya vizuri uwanjani na ikaibuka na ushindi kinachofuatia ni kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo ambapo watu wanakwenda kufurahia walichofanya.
Tayari shirikisho la soka nchini Uingereza FA limeiandikia Manchester United barua kuhusiana na tukio hilo ambapo inadaiwa kwamba kulikuwa na vitendo vya urushwaji wa chupa za maji na maziwa kati ya pande hizo mbili.
No comments:
Post a Comment