Vijijji vya Kwamtoro, Sanzawa na Mangasta vilivyopo Dodoma Wilaya ya
Chemba wamepata neema ya Maji safi na salama baada ya mfadhili kutoka
Abu Dhabi Bwana Jamal Mohamed kutoa msaada wa visima 4 vya Maji safi na
salama kwa wananchi hao.
Bwana Jamal Mohamed alipata ujumbe kuwa Maeneo hayo kunashida ya Maji
safi ndipo akaamua kujitolea kuwasaidia wananchi hao kwa kuwachimbia
visima 4 vyenye urefu wa mita 150 kwenda chini vyenye thamani ya milion
35 kwa kila kimoja.
Mpaka sasa visima 3 vishakamilika na kimoja ndio kimeanza kuchibwa, Jumla ya msaada huo utagharimu milion 140 za kitanzanai.
Wananchi wameelezea furaha yao juu ya msaada hou nakudai kuwa shida ya
maji ilikuwa nitatizo kubwa sana katika maeneo hayo ili kupata maji ili
kuwa nilazima utembee kilometa 10 mpaka 15.
Kwa mujibu wa waataalamu wa kuchimba visima wanasema visima hivyo kila
kimoja kinatoa lita 15,000 kwa saa na kwa mujibu wa wakazi wa maeneo
hayo kutakuwa hakuna tena shida ya maji safi na salama.
Jumla ya visima vyote vitatoa maji lita laki 2 mpaka 3 kwa siku ambazo zitaweza kuhudumia watu zaidi ya 2000 mpya 3000 kwa siku.
No comments:
Post a Comment