H-R McMaster alikuwa akizungumza katika mkutano wa ulinzi mjini Carlifonia ambapo alionya uwezekano wa vita dhidi ya Korea Kaskazini unaendelea kuongezeka kila uchao, Hata hivyo aliongezea kuwa kuna njia za kutatua mzozo huo bila ya kutumia vita.
Ameitaka China kuiwekea vikwazo vya mafuta taifa hilo ili kufanya kuwa vigumu kwa Pyongyang kujaza mafuta makombora yanayofanyiwa majaribio, Korea Kaskazini imeishutumu Marekani kwa kuchochea vita.
Imetaja zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Korea kusini na Marekani kuwa la uchochezi na kwamba linaweza kusababisha vita.
No comments:
Post a Comment