Ombi la amri ya zuio liliwasilishwa na chama cha Liberty (LP) ambacho kinadai kulikuwa na udanganyifu na dosari wakati wa uchaguzi wa Oktoba 10 ambazo zinasababisha matokeo ya uchaguzi yafutwe.
Aidha, chama tawala cha Unity Party pamoja na All Liberian Party na Alternative National Congress vinejiunga katika shauri hilo la Liberty Party.
Mjadala huo miongoni mwa majaji wa Mahakama ya Juu ulifanyika kwa zaidi ya saa mbili. Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa wakiwemo kutoka Taasisi ya Taifa ya Demokrasia (NDI), Umoja wa Ulaya, mtandao wa waangalizi kutoka Liberia na wengineo walionekana kwenye ghorofa ya tatu ya jengo hilo.
Wanahabari na waangalizi hao hawakuruhusiwa kufika ghorofa ya tatu ya Hekalu la Haki ambao majaji walikuwa wakijadili masuala ya haki.
Ikiwa mahakama itaridhia kuweka amri ya zuio ina maana Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haitaweza kuendelea na maandalizi ya uchaguzi wa marudio Novemba 7 kama ilivyopangwa.
No comments:
Post a Comment