Tuesday, 7 November 2017

Trump ataka mazungumzo na Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka Korea Kaskazini kuja kwenye mazungumzo kujadili suala la kuondoa silaha za nyuklia.
Bwana Trump alikuwa akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari na mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae-in mjini Seoul kama sehemu ya ziara yake barani Asia.
Mapema Trump alikuwa ametishia hatua kali za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini.
Yuko kwenye ziara ya nchi tano barani Asia ambapo programu za nyuklia za Korea Kaskazini zimekuwa kwenye ajenga.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Trump na Moon walirejelea wito wao kwa Korea Kaskazini kuachana na mipango yake ya nyuklia akisema kuwa ni jambo bora kwa Korea Kaskazini kuja kwa mazungumzo.

Licha ya Marekani kupeleka wanajeshi wengi eneo hilo, Trump alisema kuwa ana matumaini kwa Mungu kuwa hatachukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini.

Viongozi hao wawili pia walitoa wito kwa China na Urusi kuishinikiza Korea Kaskazini.

Trump pia alisema kuwa Korea Kusini itaagiza vifaa vya kijeshi kutoka Korea Kaskazinia vya gharama ya mabilioni ya dola.
Haijulikani ikiwa makubaliano hayo tayari yalikuwa yameafikiwa lakini Bw. Moon alisema kuwa walikuwa wamekubaliana kuanza mazunguznoa hayo ili kuboresha uwezo wa ulinzi wa Korea Kusini.
Licha kuwa Trump atakuwa nchini Korea Kusini kwa muda wa saa 24, itakuwa ziara muhimu zaidi kwa nchi hizo zote anazozuru barani Asia.
Ziara hiyo ina lengo la kuboresha ushirikiano wa kijeshi ambao umeilinda kwa muda mrefu Korea Kaskazini na ndio ujumbe wanaotaka kutuma kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Maandamano ya kumkrabisha Trump na ya kumpinga yamefanyika mjini Seol na kwingineko.
Bwana Trump ataelekea nchini China, Vietnam na kisha Ufilipino.

No comments:

Post a Comment