Makubaliano hayo ya Paris yanaunganisha mataifa duniani katika kukabiliana na hali ya tabia nchi.
Syria na Nicaragua yalikuwa mataifa ya pekee nje ya makubaliano hayo wakati yalipotiwa saini 2015.
Nicaragua ilitia saini yake mnamo mwezi Oktoba.
Mnamo mwezi Juni Marekani ilisema kuwa itajiondoa , lakini sheria za mkataba huo zinasema kuwa hatua hiyo haiwezi kufanyika hadi 2020.
Wakati huohuo maafisa wa Ufaransa wamesema kuwa rais Donald Trump hakualikwa katika mkutano wa wa Disemba kuhusu hali ya tabia nchi utakaofanyika mjini Paris.
Zaidi ya mataifa 100 yamealikwa katika mkutano huo ambao unalenga kujenga miungano ya kifedha na kibishara ili kuimarisha mkataba huo kulingana na msaidizi wa rais Emmanuel Macron.
Akitangaza uamuzi huo wa Marekani mnmao mwezi Juni, rais Trump alisema kuwa ni wajibu wake kuilinda Marekani na kwamba atakubaliana na mkataba mpya ambao hautaathiri biashara za Marekani.
Alidai kwamba mkataba huo utagharimu kazi milioni 6.5 za Wamarekani na dola trilioni 3 za uchumi wake, huku washindani wake wakuu kama vile China na India wakipendelewa na makubaliano hayo.
Taarifa ya Marekani iliotolewa mwezi Oktoba baada ya Nicaragua kutia saini makubaliano hayo ilisema kuwa Marekani itajiondoa hadi pale mkataba huo utakapoipendelea.
Msemaji wa Ikulu ya Whitehouse Kelly Love amesema kuwa hakuna mabadiliko yoyote kuhusu msimamo huo.
No comments:
Post a Comment