Sumaye ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye mkutano Kimara jijini
Dar es salaam alipokuwa akimnadi mgombea udiwani wa CHADEMA, na kusema
kwamba hali ya uchumi na maisha ya wananchi kwa sasa ni mbaya zaidi,
lakini iwapo wakisema ukweli wanaonekana ni waongo hivyo sio suala la
kuendelea kulifumbia macho na kuacha CCM iendelee kutawala.
"Hatuwezi kukubali CCM iendelee kutawala nchi hii wakati watu wanazidi
kuwa na hali mbaya ya maisha, tukiwaambia watu wana hali mbaya wanasema
tunasema uongo, tukisema uchumi umezama wanasema tunasema uongo, kama
tunasema uongo kwa nini hali za wananchi zinakuwa mbaya, maana kuna vitu
ambavyo havijifichi, kama uchumi unakwenda vizuri tafsiri zake
itaionekana kwenye hali ya wananchi, hali ya wananchi ni mbaya", amesema
Sumaye.
Hivi karibuni kumekuwa na mvutano kati ya vyama vya upinzani kudai kuwa
uchumi wa nchi umeshuka, huku serikali ikikanusha na kuoa taarifa kuwa
suala hilo halina ukweli wowote, kwani uchumi wa nchi umetengemaa
kutokana na kubana matumizi.
No comments:
Post a Comment