Timu ya taifa ya Morocco imekata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la
Dunia mwakani nchini Urusi baada ya kuwapiga wenyeji, Ivory Coast mabao
2-0 mjini Abidjan.
Simba wa Atlas waliingia kwenye mechi hiyo Uwanja wa Felix
Houphouet-Boigny wakiwa wanawazidi pointi moja Tembo wa Ivory Coast na
walihitaji sare tu ili kupata nafasi ya kwenda Urusi mwakani.
Hata hivyo, mabao mawili ndani ya dakika tano kutoka kwa Nabil Dirar na
Medhi Benatia yaliwapa ushindo mzuri katika mechi hiyo ya Kundi C.
No comments:
Post a Comment