Baraza la habari Tanzania (MCT)
limewataka wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari kuweka wazi sera na
taratibu za vyombo hivyo kwa waandishi wao ili kuwaepusha na vikwazo
,usumbufu,na madhara pindi wawapo kwenye kazi zao.
Hayo yamezungumzwa na Katibu
Mtendaji wa Baraza hilo Bw.Kajubi Mukajanga alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
kupinga jinai dhidi ya wanahabari yaani(International Day to end
impunity for crime Against journalists) ambapo amewataka wamiliki na
wahariri kuziweka wazi sera za vyombo vyao ili kuwasaidia waandishi wao
kujua nini wanatakiwa kukiandika au kukichapisha ili kisilete madhara na
migogoro katika jamii kwakufanya hivo itasaidia kupunguza madhira
wakiwa kazini.
Aidha Bw.Mukajanga amewakumbusha
viongozi wa vyombo vya habari hususani wamiliki,watendaji wakuu na
wahariri wajibu wao wa kuwalinda waandishi wao na kuzingatia usalama
wao.
Hata hivyo Bw.Mukajanga ameasa
vyombo vya habari visipuuze sheria zilizopo kwani hata kama ni mbaya na
ngumu kwa kiasi gani lakini zipo na zinaweza kufanyiwa kazi wakati
wowote pia amesisitiza juhudi za pamoja ziimarishwe kuhakikisha kuwa
sheria hizo mbaya zinafutwa au kufanyiwa marekebisho.
No comments:
Post a Comment