Wednesday, 8 November 2017

Lugola, amewataka wananchi kutoitafriri vibaya kauli ya Rais kufanya shughuli za kilimo kwenye vyanzo vya maji

Naibu waziri wa Mungano na Mazingira Kangi Lugola, amewataka wananchi kutoitafriri vibaya kauli ya Rais kuhusu kufanya shughuli za kilimo kwenye vyanzo vya maji, na kusema kwamba hakuna sheria inayoruhusu watu kufanya shughuli za kilimo.
Waziri Lugola ameyasema hayo leo alipokuwa akijibu swali Bungeni kuhusu kauli hiyo ya Rais ambayo imeonekana kuruhusu watu kufanya uharibifu kwenye vyanzo vya maji na mazingira, na kusema kwamba

“Niwahakikishie kauli ya Rais isije ikapotoshwa wananchi wakaenda kuvamia maeneo ya mito na kuanza kulima, na kauli aliyoitoa Mheshimiwa Rais, Watanzania waelewe vyanzo vya maji ndio uhai wetu, hakuna anayeruhusiwa kwenda kwenye chanzo cha maji, kwa hiyo hamruhusiwi .", Amesema Kangi Lugola
Naibu Waziri Kangi Lugola ameendelea kwa kusema kwamba yeyote atakayevunja sheria na kuingia kwenye vyanzo vya maji atachukuliwa hatua, lakini pia ifahamike kwamba Rais ana mamlaka ya kuruhusu watu kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria ya mita 60.
"Yeyote atakayevunja sheria hatasalimika, sheria niliyoisema ya 2004 Rais anaweza akatoa Kibali, Waziri anaweza akatoa kibali kwenye maeneo ya mita 60 kutokana na changamoto aliyoiona, kwa hiyo Rais hajavunja sheria, na ninyi mtakapowachochea wananchi kuvunja sheria, sheria za Rais Magufuli mtapambana nazo", amesema Kangi Lugola.


Hapo Jana Rais Magufuli alipokuwa kwenye ziara yake mkoani Kagera, ameitaka serikali kuwaacha vijana wanaofanya shughuli za kilimo kando ya mto wa maji kwani wanajiiingizia kipato.

No comments:

Post a Comment