Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa leo Ijumaa kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Wakili aomba kesi ya utakatishaji fedha dhidi ya akina Kitilya ifutwe
Pia ameeleza kuwa bado wanasubiri awamu ya pili ya upelelezi kutoka nchini Uingereza, kutokana na hilo ameomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Baada ya ombi hilo Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 10, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
No comments:
Post a Comment