Bodi imeziandikia barua timu zote 16 za ligi kuu kuzifahamisha juu ya Singida United kuhama kutoka uwanja wa Jamhuri Dodoma ambao ilikuwa inautumia kama uwanja wake wa nyumbani na sasa itarejea Singida kwenye uwanja wa Namfua.
Uwanja huo wa Namfua utaanza kutumika Jumamosi hii Novemba 4 kwenye mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara raundi ya 9 ambapo Singida United itacheza na mabingwa watetezi Yanga.
Singida United wamewaaga rasmi mashabiki wao wa mkoani Dodoma na kuwatakia kila la kheri na timu yao ya Dodoma FC wakiwaombea ipande daraja ili mwakani waweze kushuhudia uhondo wa Ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment