Mfanyakazi katika kampuni ya mtandao wa kijamii wa Twitter, ameifunga akaunti ya Rais wa Marekani Donald Trump, @realdonaldtrump, kitendo ambacho kimeelezwa na kampuni hiyo kuwa ni makosa ya kibinadamu yaliyofanywa na mfanyakazi wao.
Twitter imeeleza kuwa akaunti ya Rais Trump yenye jina @realdonaldtrump iliondolewa juzi Alhamisi kwa muda wa dakika 11 na mfanyakazi ambaye alikuwa amebakiza muda mfupi wa kufanya kazi katika kampuni hiyo.
Kwa sasa akaunti y Rais Trump imesharejeshwa hewani na haikupata madhara yoyote.
Twitter imesema kuwa inachunguza tatizo hilo na kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa kisa kama hicho hakitokei tena.
Rais Trump ambaye ana wafuasi zaidi ya 41 milioni na ni mtumiaji mkubwa wa mtandao wa twitter, hajasema lolote kuhusu kufungiwa kwa akaunti yake.
No comments:
Post a Comment