Sunday, 12 November 2017

Almasi ya thamani kubwa yapatikana nchini Sierra Leone

Wachimba migodi nchini Sierra Leone wamepata almasi ya karati 476 ambayo inatajwa kuwa ya 29 kuwai kupatikana duniani.
Wataalamu bado hawana uhakika inaweza kuwa ya thamani ya kiasi gani.
Hii ni miezi minane baada ya almasi ya zaidi ya karati 700 kupatikana ambayo ni kabwa zaidi kuwai kupatikana nchini Sierra Leone kwa nusu karne.
Jiwe hilo linatarajiwa kuuzwa kwenye mnada mjini New York mwezi ujao.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la madini nchini Sierra Leone alisema kuwa kupatikana kwa almasi hiyo kunaonyesha umuhimu wa mkoa wa Kono ambapo almasi hizo zote zimepatikana.
Nchi hiyo ina matumaini ya kutumia mnada huo wa mwezi Desemba kujikwamua kutoka vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 11 ambavyo vilichangiwa na biashara ya almasi.

No comments:

Post a Comment