WIZARA ya Habari, Utamaduni, Utalii na
Michezo imeeleza kuwa itahakikisha inaingia katika mfumo wa utangazaji
wa Dijitali kwani maendeleo katika ujenzi wa miundombinu yake yanatia
moyo na vifaa vyote vinatarajiwa kufika na kufungwa kabla ya Disemba 31
mwaka huu.Maelezo hayo yametolewa na uongozi wa Wizara hiyo, wakati wa
mkutano kati ya uongozi huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika kuangalia utekelezaji wa
Malengo Makuu ya Wizara hiyo kwa kipindi cha Aprili- Juni 2011-2012 na
Julai- Septemba 2012-2013.
Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar ambapo pia, Makamu
wa Kwanza wa Rais Maalim Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi
Seif Ali Idd na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu
Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee walishiriki kikamilifu
Akisoma taarifa ya utangulizi ya utekelezaji wa Malengo makuu hayo ya Wizara