Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Mahmoud Mgimwa |
HIFADHI ya Taifa ya Ngorongoro imetajwa kuwa ipo hatarini kutoweka, kutokana na mwingiliano wa watu kuwa mkubwa huku idara nyingi zikiongozwa na watu wasiostahili kuongoza. Aidha, Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Mahmoud Mgimwa ametoa rai kwa Wizara ya Nishati na Madini kuhakikisha haitoi tena vibali vinavyomaliza muda wake ndani ya Hifadhi ya Ziwa Manyara na hifadhi nyingine ambazo baadhi ya wachimbaji wanachimba madini ya aina mbalimbali. Kauli hizo zilitolewa jana kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli na Mgimwa wakati walipokuwa wakihitimisha ziara iliyofanywa na kamati hiyo iliyokuwa ikitembelea maeneo mbalimbali mkoani Arusha, kujionea uharibifu wa mazingira, na migogoro ya ardhi kwenye Hifadhi mbalimbali za Taifa. Akisoma maazimio na maagizo hayo mbele ya wanahabari waliofuatana na kamati hiyo, Lembeli alisema Hifadhi ya Ngorongoro ipo hatarini kutoweka, kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo, pia suala la wakuu wa idara kuondolewa nalo pia linachangia hifadhi hiyo kufa. Alisema ingawa haingilii maamuzi ya Bodi ya Ngorongoro, lakini asilimia 80 ya wakuu wa idara hawapo na idara nyingi zinaongozwa na watu wasiostahili kuongoza. Alisema Ngorongoro ina matatizo makubwa hivyo ni lazima serikali iwe makini kuhakikisha hifadhi hiyo haifi. Kuhusu suala la uchimbaji wa madini ndani ya hifadhi hiyo, Lembeli alisema kamati imetembelea hifadhi hiyo na kujionea uharibifu mkubwa wa mazingira kwani baadhi ya wachimbaji wanachimba madini kisha hawafukii mashimo. Alisema ni vyema sasa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Nishati na Madini, kuacha kutoa vibali vilivyokwisha muda wake kwa ajili ya uchimbaji wa madini kwani mazingira yanaharibiwa. Mgimwa alisisitiza kuwa kuanzia sasa hakuna uchimbaji wa madini utakaoendelea na kwa wale wanaoendelea kuchimba madini hayo, watazungumza na Wizara ya Nishati na Madini ili kuangalia vibali vyao na leseni zao zitakapoisha muda wake, hawataruhusiwa tena kuchimba madini hayo ndani ya hifadhi hiyo na hifadhi nyingine za Taifa. Ndani ya Hifadhi ya Ziwa Manyara yanapatikana madini aina ya emarodi, ambayo ni moja ya madini ghali zaidi duniani na gra
No comments:
Post a Comment