Licha ya kumzidi miaka 10, Zari atangaza rasmi kuwa ni mtu wake wa karibu kwa sasa
Johannesburg/Dar. Baada ya kuukimbia ukweli kwa
kipindi cha mwezi mmoja, mwanamuziki Diamond Platnumz amethibitisha kuwa
na uhusiano baina yake na staa maarufu kutoka Uganda, Zari ‘The Boss
Lady’ na kwamba atakuwa mgeni rasmi katika hafla yake ijulikanayo ‘Zari
All White Ciroc’ itakayofanyika mwezi huu.
Nyota huyo aliyevunja rekodi kwa kunyakua tuzo
tatu za Channel O Music Video Awards (ChoMVA) wikiendi iliyopita,
amekuwa akijadiliwa katika mitandao ya Tanzania na nje ya nchi kwa
kuonekana na wanawake tofauti kila wakati, hali inayowachanganya
mashabiki wake.
Hata hivyo, Diamond hajasita kuelezea hisia zake
za sasa na kwamba yupo tayari kuhudhuria hafla hiyo, inayotarajiwa
kufanyika Desemba 18.
“Nitakuwapo katika hafla hiyo, ni lazima nimuunge
mkono, mbona kuna wengi wanaunga mkono na watu hawasemi, kama wanavyokaa
kimya kwa wengine na huku iwe vivyo hivyo,” alisema Diamond huku
akishindwa kukiri moja kwa moja kwamba ana uhusiano na Zari, “waswahili
wanasema A na B yote majibu.”
Kwa upande wa Zari ambaye ndiye aliyekuwa
msindikizaji mkuu wa Diamond wakati wa utolewaji wa tuzo hizo,
alitangaza rasmi kwamba nyota huyo ndiye atakayekuwa mgeni rasmi katika
hafla yake.
“Habari mpya ni kwamba Diamond Platnumz atakuwa
mgeni rasmi katika pati ya Zari All White Ciroc, najihisi niko sahihi
kwa sababu sioni kama kuna ushindani wowote, huyu ni mtu wangu na
itabaki kuwa hivyo,” alisema Zari.
Zari ni nani?
Jina lake halisi anajulikana kama Zarinah Hassan
maarufu Zari. Alizaliwa Septemba 23, 1980 huko Jinja, Uganda, kati ya
shule alizosoma ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jinja.
Alikwenda Kampala na baadaye jijini London ambako alipata Diploma ya
Cosmetology.
Zari alianza kujishughulisha na masuala ya muziki
akiwa shule ya msingi. Kwa kuungwa mkono na familia yake mwaka 2007,
alirekodi wimbo wa kwanza Oliwange (Wewe ni Wangu), albamu hiyo ilimpa
tuzo Channel O ikiwa video bora ya Afrika Mashariki. Tangu hapo alitoa
vibao kadhaa.
Mwanamuziki huyo ambaye ana asili ya India,
Burundi, Uganda na Somalia, mwaka 2009 alipata tuzo ya mwanamuziki bora
wa kike, huku mwaka 2008 akishinda tuzo ya Channel O akiwa mwanamuziki
bora Afrika Mashariki.
Usiyoyajua kuhusu Zari
No comments:
Post a Comment