Mshambuliaji wa Barcelona,Lionel Messi (katikati) akiwakimbiza wachezaji wa Chelsea wakati wa mechi ya nusu fainali kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya,Aprili mwaka huu. |
LONDON, England
LIONEL Messi amerejea kileleni katika orodha ya wachezaji 10 bora inayotolewa na AP Global baada ya kuvunja rekodi iliyowekwa miaka 54 iliyopita na Pele, huku Bayern Munich kiongoza katika klabu bora.
Katika orodha hiyo inayochapishwa kila baada ya wiki moja na The Associated Press, Messi amemwacha kwa mbali mpinzani wake, mshambuliaji wa Mexico, Javier Hernandez, ambaye amekuwa kwenye kiwango cha juu cha ufungaji ndani kwa Manchester United wiki iliyopita.
Messi sasa anahitaji kufunga mabao 10 tu mwaka huu ili aweze kuvunja rekodi iliyowekwa na gwiji wa Ujerumani, Gerd Muller mwaka 1982.
LIONEL Messi amerejea kileleni katika orodha ya wachezaji 10 bora inayotolewa na AP Global baada ya kuvunja rekodi iliyowekwa miaka 54 iliyopita na Pele, huku Bayern Munich kiongoza katika klabu bora.
Katika orodha hiyo inayochapishwa kila baada ya wiki moja na The Associated Press, Messi amemwacha kwa mbali mpinzani wake, mshambuliaji wa Mexico, Javier Hernandez, ambaye amekuwa kwenye kiwango cha juu cha ufungaji ndani kwa Manchester United wiki iliyopita.
Messi sasa anahitaji kufunga mabao 10 tu mwaka huu ili aweze kuvunja rekodi iliyowekwa na gwiji wa Ujerumani, Gerd Muller mwaka 1982.
''Messi amefika kileleni kutokana na uwezo wake wa kuvunja rekodi,'' alisema James Porteous wa gazeti la The South China Morning Post nchini Hong Kong. ''Amevunja rekodi ya Pele ya kufunga mabao 75 kwa mwaka moja alipofunga magoli mawili dhidi ya Mallorca. Anahitaji mabao 10 katika michezo 10 iliyobaki mwaka huu ili kuipita rekodi ya Gerd Muller ya mabao 85 na hakuna shaka kama ataweza kufikia hilo.''
Mike McGrath wa Uingereza ni mwandishi wa Wardles News Agency na Gazeti la The Sun, alisema: ''kama kuna ubishi kuhusu Lionel Messi kuwa ni mchezaji bora wa dunia, sasa umekwisha kwa kuivunja rekodi ya Pele. Amekuwa akitegeneza rekodi mpya kila wiki.''
Kila mwandishi wa AP kura yake inatoa pointi 10 kwa mchezaji bora wa wiki, pointi hiyo inaweza kupungua kama akichagua mchezaji mwingine. Sawa na inavyokuwa kwenye klabu.
Mshambuliaji wa Juventus, Fabio Quagliarella amepanda hadi nafasi ya tatu baada ya kufunga mabao manne katika mechi mbili.
Messi amepata pointi 139, Hernandez (98) na Quagliarella (67).
Kipa Fraser Forster aliyekuwa shujaa wa Celtic kwenye mchezo walioshinda wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona, waandishi hao walimpigia kura na kushika nafasi ya nne akipata pointi 61. Mshambuliaji Edinson Cavani (5), Franck Ribery (6), Cristiano Ronaldo (7) na Marouanne Fellaini (8) wote kutokana na mabao yao waliofungwa.
''Cavani amechukua nafasi ya Radamel Falcao kuwa ni mshambuliaji hatari zaidi Ulaya,'' Will Tidey wa Bleacher Report la Marekani alisema. ''Mshambuliaji huyo wa Uruguay amefunga mabao yote manne ya Napoli katika Europa Ligi, pia alifunga moja na kutegeneza jingine katika Serie ëAí siku ya Jumapili.''
Ronaldo aliyeifungia Real Madrid bao dhidi ya Levante pamoja na kuwa amepasuka jicho ameshika nafasi ya saba.
Bayern imekuwa timu bora ya wiki kwa kupata pointi 128, wakitokea nafasi ya tatu. Bayern ilishinda 6-1dhidi ya Lille kwenye Ligi ya Mabingwa, pia ikishinda 2-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt mwishoni mwa wiki na kuendelea kubaki kileleni mwa Bundesliga.
Juventus ilijirekebisha baada ya kufungwa Inter Milan wakiwa wamefunga mabao 10, katika michezo miwili na kushika nafasi ya pili kwa pointi 121. Mabingwa hao wa Italia, walishinda 4-0 katikati ya wiki dhidi ya miamba ya Denmark, Nordsjaelland, pia walifunga mabao sita dhidi ya Pescara.
Manchester United ipo nafasi ya tatu, baada ya mafanikio katika Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu shukrani kwa Hernandez.
Ushindi wa Celtic wa katikati ya wiki dhidi ya Barcelona umewafanya wapande hadi nafasi ya nne, ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu ya Scotland kuingia kwenye kumi bora.
Barcelona wameporomoka hadi nafasi ya nne baada ya kipigo cha Celtic. Mabingwa wapya wa Brazil, Fluminense wenyewe wanakamata nafasi ya sita kwenye 10 bora.
Wachezaji bora
1. Lionel Messi, 139 pointi.
2. Javier Hernandez, 98.
3. Fabio Quagiarella, 67.
4. Fraser Forster, 61.
5. Edinson Cavani, 59.
6. Franck Ribery, 54.
7. Cristiano Ronaldo,39.
8. Marouanne Fellani, 35.
9. Marco Reus, 34.
9. Willian, 34.
Timu:
1. Bayern Munich, 128 pointi.
2. Juventus, 121.
3. Manchester United, 119.
4. Glasgow Celtic, 99.
5. Barcelona, 79.
6. Fluminense, 70.
7. Borussia Dortmund, 58.
8. Real Madrid, 42.
9. Manchester City, 31.
10. Chelsea, 27
No comments:
Post a Comment