Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (kushoto) akijaribu kumpiga
chenga beki wa Black Leopards, Muganga Jean katika mechi ya kirafiki
kwenye Uwanja wa Taifa jana. Picha na Michael Matemanga
IKICHEZA soka lenye ‘harufu’ ya Uturuki, Yanga jana
iliwathibitishia mashabiki wake ilichojifunza Ulaya baada ya kuiogesha
kichapo cha mabao 3-2 Leopards ya Afrika Kusini katika mchezo wa
kirafiki wa kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga ilirejea nyumbani mwanzoni mwa wiki hii
baada ya wiki mbili za kujifua nchini Uturuki ilikocheza mechi tatu,
ikifungwa mbili na sare moja.
Jana Yanga ilikuwa tofauti na ilivyozoeleka awali kufuatia kuonyesha soka lenye ‘taaluma’ na kuwapeleka puta Chui kutoka Bondeni.
Jana Yanga ilikuwa tofauti na ilivyozoeleka awali kufuatia kuonyesha soka lenye ‘taaluma’ na kuwapeleka puta Chui kutoka Bondeni.
Ingawa mchezo huo ulipooza dakika 10 za mwanzo
kutokana na kila upande kujaribu kumsoma mwenzake, ulianza kuchangamka
ndani ya robo ya kipindi cha kwanza.
Dakika ya 10, nusura Didier Kavumbagu atikise
nyavu za Chui hao wa Bondeni kama siyo shuti lake kali kutikisa mwamba
wa goli, huku pia akishindwa kufunga dakika ya 22 kufuatia shuti lake
kuchezwa na kipa.
Mbuyu Twite angeweza kufunga kwa upande wa Yanga
katika dakika ya 25, lakini shuti lake la karibu na lango lilichezwa na
kipa wa Leopards.
Shambulizi lingine kali kwenye lango la Leopard
lilifanywa dakika ya 52 baada ya wachezaji wa Yanga kushirikiana vizuri
lakini wakaishia ‘kumpasia’ mpira mkononi kipa. Leopards wangeweza
kusawazisha bao hilo baada ya shuti la Rodney kugonga mwamba wa Yanga
dakika ya 24, na akashindwa kufunga tena dakika ya 33 baada ya Ally
Mustapha kudaka shuti lake.
Leopards walirejea na kasi kipindi cha pili na
kufunga bao la kusawazisha kupitia kwa Humphery Khoza akiunganisha kona
ya Abbas Amidu, na kisha kufunga bao la pili dakika ya 88 kwa mkwaju wa
penalti kupitia Romagalela baada ya Nadir Haroub kumwangusha ndani ya
eneo la hatari Khoza.
Frank Domayo aliifungia Yanga bao la pili dakika
ya 63 akimalizia pasi ya Niyonzima, kabla ya Tegete kufunga bao la tatu
kwa shuti kali akiwa nje ya 18.
Tegete aliyeng’ara safari ya Uturuki, aliipeleka Yanga mapumziko ikiwa mbele baada ya kufunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 33.
Tegete aliyeng’ara safari ya Uturuki, aliipeleka Yanga mapumziko ikiwa mbele baada ya kufunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 33.
Kiki hiyo ya penalti ilitolewa na mwamuzi baada ya
beki wa Leopards, Nkoyiyabu Xakane kumfanyia madhambi Niyonzima ndani
ya eneo la hatari. Kocha Ernets Brandts aliwapumzisha, mapacha Twite na
kipa Mustapha na Tegete na kuingia Msuva, Juma Abdul, George Banda na
kipa, Said Mohamed.
Wakati huohuo, Mkutano wa wanachama wa klabu ya
Yanga, ufanyika leo kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay Dar es
Salaam huku ajenda kuu ikiwa kuzungumzia mapato na matumizi ya klabu.
Yanga ilikuwa katika mgogoro wa uongozi kabla ya kufanya uchaguzi wake Julai 15 mwaka jana.
Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema
jana kuwa, mkutano huo utaanza saa 3:00 asubuhi na kusisitiza wanachama
wanapaswa kuwahi ili kwenda na muda.
Kizuguto alisema miongoni mwa mambo watakayozungumzia pia ni ushiriki wa timu yao wakati mzunguko wa pili wa ligi kuu ukikaribia. Ligi Kuu inatarajia kuanza Januari 26.
Pia ajenda ya mengineyo itakuwa kufahamu idadi ya wanachama hai waliolipia kadi zao kwa wakati.
Kizuguto alisema miongoni mwa mambo watakayozungumzia pia ni ushiriki wa timu yao wakati mzunguko wa pili wa ligi kuu ukikaribia. Ligi Kuu inatarajia kuanza Januari 26.
Pia ajenda ya mengineyo itakuwa kufahamu idadi ya wanachama hai waliolipia kadi zao kwa wakati.
No comments:
Post a Comment