WIZARA ya Habari, Utamaduni, Utalii na
Michezo imeeleza kuwa itahakikisha inaingia katika mfumo wa utangazaji
wa Dijitali kwani maendeleo katika ujenzi wa miundombinu yake yanatia
moyo na vifaa vyote vinatarajiwa kufika na kufungwa kabla ya Disemba 31
mwaka huu.Maelezo hayo yametolewa na uongozi wa Wizara hiyo, wakati wa
mkutano kati ya uongozi huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika kuangalia utekelezaji wa
Malengo Makuu ya Wizara hiyo kwa kipindi cha Aprili- Juni 2011-2012 na
Julai- Septemba 2012-2013.
Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar ambapo pia, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee walishiriki kikamilifu
Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar ambapo pia, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee walishiriki kikamilifu
Kwa upande wa Shirika la Magazeti ya Serikali, limekuwa likitekeleza majukumu yake vizuri na tayari lemeanza uchapishaji wa gazeti jengine jipya la Utamaduni na Michezo.Uongozi huo ulieleza kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika uendelezaji wa gazeti hilo jipya na limepokelewa vizuri hasa kwa upande wa Unguja na Pemba kutokana na taarifa zake.Ukieleza kuhusu mafanikio yaliopatikana kwenye gazeti mama la Zanzibar Leo, uongozi huo ulieleza kuwa mauzo yake yanatia moyo sana na limekuwa likionesha mafanikio makubwa katika mauzo ikilinganisha na ilivyokuwa hapo siku za nyuma.Kwa upande wa sekta ya utalii, uongozi huo ulieleza kuwa juhudi zinachukuliwa katika kuimarisha sekta hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa katika kuimarisha uchumi nchini.
Tume ya Utangazaji kwa maelezo ya Wizara hiyo nayo hivi sasa inaenda vizuri baada ya kupata ufumbuzi wa kuwa na Bodi yake huku ikieleza mikakati iliyoweka katika kukiimarisha Chuo chake cha Habari ili kiweze kufikia malengo iliyojiwekea.Kwa upande wa sekta ya utamaduni na michezo, uongozi huo ulieleza juhudi na mikakati iliyojiwekea katika sekta hiyo huku ikieleza kusikitishwa kwake na kulikotokana na timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kukosa kutimiza kiu ya Rais Dk. Shein ya kuja na kombe la Challenge hapa Zanzibar mwaka huu, na kueleza mafanikio ya sekta ya michezo.Pamoja na hayo, Wizara hiyo ilieleza changamoto kubwa iliyoipata kutokana na kuporomoka kwa jengo la Beit al Ajaib, ambalo ni ngome ya historia ya Zanzibar na kusisitiza kuwa jitihada inafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mji Mkongwe ya kuondoa kifusi na kuweka miega ili kunusuru hali kabla kuanza matengenezo.
Nae, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipongeza juhudi za Wizara hiyo na kusisitiza haja ya kuendeleza juhudi katika kufikia malengo yaliyowekwa na Wizara hiyo katika sekta zake.Kwa upande wa Sekta ya Utalii, Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeamua kwa makusudi kuongeza nguvu katika kuutangaza utalii wake kwa kutambua umuhimu na thamani yake katika kuongeza pato la taifa na kukuza uchumi kwa wananchi.Alisema kuwa jitihada kubwa zitaendelea kuchukuliwa katika kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii. Sambamba na hayo, alilitaka Shirika la Magazeti ya Serikali kuendelea kujiimarisha zaidi kwani tayari limeanza kuleta matumaini makubwa
No comments:
Post a Comment