Thursday, 9 July 2015

Vituo vitatu vya televisheni vyatozwa faini, vyaony

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Nkoma.
Vituo vitatu vya televisheni vimetozwa faini na kupewa onyo kwa kurusha taarifa zilizokiuka kanuni  za huduma ya utangajaji.
 
Vituo hivyo ni Chanel Ten kupitia kipindi chake cha Kanjanja Time kimepewa onyo na kutozwa faini ya Sh. milioni 2.5, Star Tv kupitia kipindi chake cha Min Buzz  kimepewa onyo na faini ya Sh. 500, 000 na Tanzania Broadcasting Corporation (TBC1) onyo na faini ya Sh. 500, 000 kwenye mojawapo wa taarifa za habari zilizorushwa na kituo hicho.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,  Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Margeret Munyangi,  alisema wameamua kuchukua hatua hizo baada ya kamati hiyo kukaa na kujadili ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005.
 
Alisema Mei 30, mwaka huu,  kituo cha Chanel Ten kupitia kipindi cha Kanjanja Time kilichorushwa hewani kuanzia saa 2:45 hadi saa 3:10 usiku   taarifa iliyoonyesha picha ya mgonjwa akiwa katika wodi ya Hospitali ya Serikali mjini Songea huku sehemu ya makalio yake yakiwa wazi na kuonyesha vidonda.
Pia kipindi hicho kilionyesha taarifa ya walemavu wawili wakipigana hadharani huku watangazaji  wakishangilia na kukirudia mara kadha na uchochezi dhidi ya serikali kwa madaktari  ili wafukuzwe na hospitali hiyo ifungwe.
 
“Hii ni kinyume cha kanuni za huduma ya utangazaji (Maudhui), 2005  katika kanuni Na. 5(c), (h) na 9(1),” alisema Munyangi.
 
Aliongeza kuwa kipindi hicho kilionyesha taarifa ya watu  wenye ulemavu ambao walikuwa wanapigana hadharani na mtangazaji wa kipindi alisikika akishabikia kitendo hicho huku akifananisha na pambano la ngumu za kulipwa.
Munyagi alisema kitendo hicho ni kinyume cha kanuni za huduma ya utangazaji (maudhui), 2005 . Na. 18(1), (b), (i), (ii) na (iii).
 
“Kituo hiki kimekiuka kanuni  za huduma za utangazaji (maudhui) 2005 Na. 5(c), (h), 9(1), 18(1) (b),(i),(ii) na (iii) ambazo  baadhi ya kanuni hizo ni  tano. Kila mwenye leseni ya utoaji huduma za utangazaji lazima ahakikishe kuwa vipindi vyake vinazingatia (c) ubora wa vipindi pamoja na staha,” alisema.
 
Kwa upande wa Star Tv,  alisema Juni 3, mwaka huu kituo hicho kilikiuka maudhui, 2005 kupitia kipindi cha Mini Buzz kilichorushwa hewani kati ya saa 12:30 jioni hadi saa 1:00 usiku.
 
Alisema kipindi hicho kilikiuka kanuni za utangazaji kwa kujadili mada iliyohusu ubakaji katika ndoa kwa muda ambao watoto hupata fursa ya kuangalia na kusikiliza.
 
Aliongeza kuwa washiriki wa kipindi hicho ambao walikuwa ndani ya gari walijadili maana ya ubakaji katika ndoa na uhalali wa mwanaume kumuingilia mkewe bila ridhaa yake huku mtangazaji  akirejea masuala hayo kama nchi ya Uganda.
 
“ Kituo hiki kimekiuka kanuni za huduma za utangazaji 2005 Na. 5(c), (g), 14(1), 16(3), 26(1) na 26(2) ambazo baadhi ya kanuni zinasomeka hivi 5(c), (g) kila mwenye leseni ya utoaji huduma za utangazaji lazima ahakikishe kuwa vipindi vyake vinazingatia (c) ubora wa vipindi pamoja na staha na (g) kuwarinda na kuwaepusha watoto kuiga tabia mbaya,” alisema. 
 
Kwa upande wa TBC1, alisema Machi 21, mwaka huu kituo hicho kilivunja kanuni za huduma ya utangazaji 2005, kupitia kipindi cha taarifa ya habari kilichiorushwa hewani kati ya saa 2:00 hadi 3:00 usiku taarifa hiyo ilionyesha mtoto wa kiume wa miaka 11 ambaye alilawitiwa na vijana wawili wenye umri wa kati ya 22 na 25.
 
Alisema kituo hicho kilionyesha utambulisho wa picha, majina ya  ya wazazi wa mtoto, mahali anapoishi na kuonekana sehemu kubwa ya mwili wa mtoto huyo na sauti yake ikisikika, hivyo kurahisisha utambuzi wake katika jamii.
 
Akisema kituo hicho kimekiuka kanuni za huduma ya utangazaji 2005, Na. 9(2), (3) zinzosomeka kuwa:
“Utambulisho wa waathirika wa ubakaji na waathirika wa makosa mengine ya ngono hautakiwi kutangazwa wazi katika kipindi bila ridhaa ya muathirika.
 

No comments:

Post a Comment