NGITILI ni eneo maalumu ambalo linatengwa kwa ajili ya kuhihadhi uoto wa asili
na misitu. Hizi ni juhudi ambazo zinafanywa katika nchi za Afrika ili kuweza
kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi hasa ukame
Nchini Tanzania katika mkoa wa Shinyanga zaidi ya wakazi 50 wamefanikiwa
kuhifadhi NGITILI baada ya mradi wa majaribio wa kupunguza uzalishaji wa hewa
ukaa unaotokana na ukataji miti hovyo na uharibifu wa misitu MKUHUMI kufanyika
kwa majaribio kuanzia mwaka 2009 hadi 2014 unaotekelezwa kwa ubia kati ya
Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa
Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kuwapa elimu wananchi hao jinsi ya
kuhifadhi NGITILI.
Mradi huo umeonekana kuwa na mafanikio baada ya NGITILI hizo kuonekana
kufanikiwa kupunguza kiwango cha hewa ukaa angani.
Mpango wa kupunguza uzalishaji hewa ukaa unaotokana na ukataji miti hovyo na
uharibifu wa misitu yaani MKUHUMI, umetekelezwa kwa majaribio kwa miaka mitano
kuanzia mwaka 2009-mpaka mwaka 2014 na umetekelezwa kwa ubia kati ya Shirika la
Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa
Misitu Tanzania yaani Mjumita. Miongoni mwa mikoa ambayo imetekeleza mradi huo
wa majaribio nchini Tanzania ni mkoa wa Shinyanga ambapo moja kati ya
utekelezaji wake ni uhifadhi wa NGITILI.
No comments:
Post a Comment