Mbunge wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi,
James Mbatia.
Amesema Makinda ameligawa vipande vipande Bunge la 10 na kutumiwa na
mhimili wa utawala.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mbatia
alisema badala ya Bunge kuisimamia serikali, lakini Makinda ameshindwa
kuliongoza Bunge hilo kutokana na shinikizo la mhimili wa utawala na kulazimika
kufuata matakwa ya CCM na hivyo kuliongoza kwa ubabe.
Alisema tofauti na ilivyokuwa katika kipindi cha Samuel Sitta na Pius
Msekwa ambao walionyesha weledi na kuliongezea heshima Bunge, lakini Makinda
ameriharibu kutokana na kuacha kusimamia Katiba ya nchi katika kuliongoza Bunge
hilo.
“Siku zote mwanamke ndiye huwa ni mtu wa mwisho kuligawa Taifa, lakini
limekuwa ni jambo la ajabu sana kuona mwanamke huyo ambaye angekuwa mstari wa
mbele katika kuitetea nchi hii, lakini ameamua lifie mikononi mwake, hata bila
kuficha ameonyesha wazi kwamba anatumika na serikali na CCM, Makinda yeye siyo
kiranja wa bunge ni mratibu tu,” alisema Mbatia.
Aliongeza: “ Badala ya Bunge kusimamia serikali kama Mhimili unaojitegemea,
limejivua kazi yake na kuwa kiungo cha serikali na inalisimamia, na ndiyo maana
hata juzi mlisikia Serikali inasema imeoliongezea Bunge siku, badala ya Bunge
lijiongezee lenyewe, hii ni fedheha.”
Mbatia alisema suala la kupelekwa bungeni kwa hati ya dharura na kujadiliwa
miswaada mitatu ya mafuta na gesi ni ajenda ya siri ya kutaka kuiweka gesi kama
dhamana ya CCM ya kupata fedha ya uchaguzi na kwamba hicho ni kiashiria cha
kuanza kuiuza nchi rejareja.
“Raslimali hizi badala ya kuwa neema kwa Watanzania, sasa inakuwa balaa,
watu wachache wanataka kuwaibia Watanzania, hivi unawezaje kuwekaje miswaada hii
muhimu kujadiliwa kwa pamoja na kuipeleka harakaharaka hivyo, sisi tumesema
hatukubali kuona hujuma hizi zinafanyika dhidi ya rasilimali na Taifa,” alisema
Mbatia.
Mbatia alisema msimamo wa Wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
uko wazi, kwamba hawako tayari kujadiliwa miswaada hiyo kwa hati ya dharura na
pia hawatashiriki wakati wa kuvunjwa bunge hilo Julai 9, mwaka huu.
Pia aliongeza kuwa hata wakiitwa katika meza ya maridhiano na Makinda
hawatakuwa tayari kushiriki.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipoulizwa juu ya taarifa
hizo za kwamba chama hicho kina ajenga ya siri ya kuifanya gesi kusaidia kuwa
dhamana katika uchaguzi, alijibu kwa kifupi kwamba ni uzushi.
No comments:
Post a Comment