.
Wajumbe wa baraza la wawakilishi wa CCM na CUF wameendelea kuvutana na kulaumiana ndani ya baraza la wawakilishi wakati wakijadili bajeti yawizara ya tawala za mikoa na idara maalum ya szm.
Hali hiyo imetokana baada ya wajumbe kuanza kuchangia wizara hiyo ambapo mwakilishi wa CCM viti maalum Mhe Mwanajuma Mdachi kuanza kuwatupia lawama wawakilishi wa CUF kuwa kazi yao ni kulalamika na hawataki kufuata sheria na ndipo mwakilishi wa CUF jimbo la Micheweni Mhe Haji Subeit naye akaanza kujibu shutuma hizo kwa ukali na kuilaumu wizara hiyo kwa kugawa majimbo na kuzuia kutoa vitambulisho kwa wananchi wanaotokakatika majimbo yao.
Akijibu hoja za upinzani wakati akijumuisha majumusiho ya wizara hiyo waziri wa nchi afisi ya rais tawala za mikoa na idara maalum za serikali Mhe Haji Omar Kheir amesema hakuna mtu anayeonewa wala kubaguliwa kinachotekelezwa ni sheria ambayo ndio anayoifuta yeye.
Bajeti ya wizara hiyo badae ilipitishwa kwa kauli moja nawajumbe wa baraza hilo huku baadhi ya wajumbe wachache wakikataa na kuipinga.
No comments:
Post a Comment