Wananchi wote wa Tanzania tunapaswa kuonyesha hisia na hasira zetu kali dhidi ya vitendo hivi vya kikatili. Bila kujali imani zetu, itikadi zetu na tofauti zozote za kijamii tunazoweza kuwa nazo lakini sasa kwa UMOJA wetu tupaze sauti kuu kabisa tuseme SASA BASI tusivumilie tena hali hii inayotia uchungu, hasira ma kujenga visasi.
Tukumbuke kwamba sisi sote ni binadamu bila kujali rangi zetu au mataifa yetu. tumetoka katika chimbuko moja tu la Adam na Eva (Hawa). Hakuna sababu ya namna yoyote ile inayofanya binadamu mmoja aishi kinyonge dhidi ya binadamu mwingine.
YAMESEMWA SANA, WALIOKEMEA WALIKEMEA SANA, WALIOONYA WAMEONYA SANA. SASA TUUNGANISHE NGUVU KAMA TAIFA TUSEME "HAPANA" UVUMILIVU UMEFIKA KIKOMO.
Serikali na mamlaka zake husika zifanye kazi zaidi na kwa kasi zaidi ya ile ya mwanzo. Hatua za makusudi za dharula zichukuliwe. Sheria dhidi ya uhalifu wa aina hii zitekelezwe mara moja dhidi ya wahusika pasipo kuwaonea huruma yoyote.
TUMECHOKA KUSIKIA VITENDO VYA KIFEDHULI KAMA HIVI NDANI YA TAIFA LETU
No comments:
Post a Comment