Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya ziara maalum
ya kukitembelea Kisiwa cha Bawe kilichopo Magharibi ya Mji wa Zanzibar
kuona shughuli za
uwekezaji katika sekta ya Utalii. Kulia kwa Balozi
Seif ni:- Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mh.
Said Ali Mbarouk.
Na Othman Khamis Ame, Visiwani
UONGOZI
wa Mradi wa uwekezaji wa sekta ya utalii unaosimamia uendeshaji wa
hoteli za Kitalii zilizomo ndani ya visiwa vidogo vidogo vya Bawe na
Changuu { Bawe leisure hotel na Changuu Leisure hotel } umehimizwa
kujitahidi kuongeza vivutio vya utalii vinavyopendwa na wageni ili
kuzidi kuimarisha mapato ya Taifa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa himizo hilo
alipofanya ziara fupi ya kukagua shughuli za uwekezaji na hifadhi ya
mazingira katika visiwa hivyo vilivyopo pembezoni mwa bahari magharibi
ya Mji wa Zanzibar.
Balozi
Seif akiambatana na Uongozi wa juu wa Wizara ya Habari, Taasisi za
mazingira, mamlaka ya uwekezaji vitega uchumi na baadhi ya maafisa wa
serikali aliueleza Uongozi wa mradi huo ulio chini ya Kampuni ya Mafuta
ya Gapco kwamba Serikali imekusudia kuimarisha sekta ya Utalii ili
ifaidishe vipato kwa pande zote husika.
Aliupongeza
Uongozi wa Bawe na Changu Leisure Hoteli kwa umakini wake katika
uendelezaji wa sekta ya utalii unaozingatia hifadhi ya maumbile ya
mazingira yaliyomo ndani ya visiwa hivyo viwili.
Msimamizi
wa mradi wa uhifadhi wa Makobe katika kisiwa cha Changuu Nd.Suleiman
Mnemo akitoa maelezo ya uhifadhi wa viumbe hao adimu duniani kwa Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyetembelea kisiwa cha
Changuu.
“
Nimefarajika na jitihada zenu za kuuendeleza mradi huu mkubwa wa
utalii. Eneo la Bawe na Changuu maumbile yake yanafanana kama Mji mpya
wa Malawi wakati unaanzishwa ukizingatia uhifadhi ya maumbile yake “.
Amesema Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza umuhimu wa Serikali na
washirika wake wote kuendelea kuongeza kasi ya uwekezaji kwenye sekta
hiyo ambayo mafanikio yake pia yanakwenda sambamba na utoaji wa nafasi
za ajira hasa kwa vijana.
Mapema
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Leisure Hoteli Bwana Freddy Tenga amesema
mradi huo wa hoteli Bawe na Changuu ulianza mnamo Mwezi Disemba mwaka
2002 kwa hatua ya matengenezo ya nyumba , huduma muhimu pamoja na
uhifadhi wa mazingira.
Bwana
Tenga amesema Uongozi wa Mradi huo umeweka mikakati ya kuimarisha
huduma zake kwa kuongeza ubora na hadhi ya vyumba na chakula ili kutoa
fursa ya mapumziko na utulivu mzuri kwa watalii na wageni wanaoamua
kuvitembelea visiwa hivyo.
Hata
hivyo Mkurugenzi wa uendeshaji wa Mradi huo wa Leisure Hotel amesema
zipo baadhi ya changamoto zinazopunguza uzuri na haiba ya visiwa hivyo
zinazotokana na uharibifu wa matumbawe.
Balozi
Seif akikagua baadhi ya majengo ya Hoteli zilizomo ndani ya kisiwa cha
Changuu wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uwekezaji katika
sekta ya Utalii . Kulia kwa Balozi ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa
Leisure Hoteli inayoendesha mradi wa hoteli Bawe na Changuu Bwana Freddy
Tenga na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali
Mbarouk.
Amesema
uharibifu huo hufanywa na baadhi ya wavuvi wanaoamua kupiga dago sehemu
hizo na huamua kutumia mitego haramu na nyavu za kukokota wakati
wanapovua hali ambayo pia huhatarisha usalama wa watalii na wageni.
Naye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk
amesema Serikali bado imelenga kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wazalendo
katika kuimarisha sekta ya uwekezaji vitega uchumi nchini.
“
Tumeshuhudia Mradi wa Leisure Hoteli unavyoendeshwa na wazalendo
ulivyokuwa mahiri katika uwekezaji ambao umelenga kuhifadhi makobe
sambamba na utunzaji wa mazingira “. Amesema Waziri Mbarouk.
Balozi Seif akikagua moja ya vyumba maridadi vilivyopo katika majengo ya Hoteli ya Leisure iliyopo Kisiwa cha Changuu.
Alifahamisha
kwamba Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo inakusudia kuandaa
mpango maalum utakaopelekwa Serikalini kwa ajili ya kuvipatia baraka za
hifadhi ya Taifa visiwa mbali mbali vya Zanzibar ikiwemo Bawe, Changuu
na Tumbatu.
Waziri
Mbarouk alieleza kwamba mpango huo ili ufanikiwe vyema taratibu
zitaandaliwa katika kuwakutanisha wawakilishi wa taasisi zote
zinazohusika na sekta za utalii, mazingira, historia, ardhi, Utalii,
Mamlaka ya uwekezaji vitega uchumi pamoja na utamaduni kwa ajili ya
kuweka mkakati wa kufanikisha mpango huo.
Mradi
huo wa uwekezaji wa sekta ya utalii unaosimamia uendeshaji wa hoteli za
Kitalii za Bawe na Changuu { Bawe leisure hotel na Changuu Leisure
hotel } tayari umeshagharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milionio
23,000,000 katika kuzifanyia matengenezo nyumba za wageni pamoja na
uhifadhi wa mazingira.
Matengenezo
hayo yamekwenda sambamba na utunzaji wa makobe wakifikia 132 hivi sasa
wakiwa katika kisiwa cha Changuu idadi inayozidi kuongezeka kutokana
na ulinzi wa kutosha uliopo katika visiwa hivyo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Kushoto akiwa pamoja na Waziri
wa anayesimamia Utalii Mh. Said Ali Mbarouk wakiangalia mazingira ya
kuvutia ndani ya eneo la Kisiwa cha Changuu.
Balozi
Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Leisure
Hoteli na watendaji wa taasisi mbali mbali za Serikali aliyofuatana nao
wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii katika Visiwa vya
Bawe na Changuu.(Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ).
No comments:
Post a Comment