Saturday, 17 October 2015

MBUNGE WA LUDEWA MHE DEO FILIKUNJOMBE AFARIKI KATIKA AJALI YA CHOPA


12105048_454521408052646_133452484_nhttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhVWnRiXNG2QtReackQvyyH2M-h222h4ICvDxPEeWP5AewzUFFrWQXO92qJOsj3ADJY4CLkPDgYP493GrD1UuhQfvqELqQuFMF-XzzbJ4USFy4fUyTnqShCuFOQwVBY5ayTBBZ3kycYKO3a/s1600/unnamed+%252861%2529.jpg



Asakari polisi na wataalamu wakikagua mabaki ya chopa namba  5Y-DKK iliyoanguka jana jioni ikitokea Dar kuelekea Ludewa sehemu ya hifadhi ya wanyama ya Selous ambapo Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe, rubani Capt. William Slaa na abiria wengine wawili - Casablanca Haule na Ngondombwitu Nkwera - walipoteza maisha.

 Timu ya waokoaji wakibeba mabaki ya miili ya marehemu


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi_WEXIC28tDO9U64J735aacyOI3PjQMYUOIMj4sezBlSG_pzggw1LxXsOH-V6Tk7ppjyF3v7EC27qZHYPwh6rAJ47JNP4N3oxGA1oDdll-ofH8D8E5SgRpDZnzvcFYM-FnD3XAxkwD3eWQ/s1600/unnamed+%252858%2529.jpg
 Askari wakiwa eneo la ajali  
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiu-cDcHFeGpehYFs4KgfiIid274cgs-OzBzSBCoDqGR8HxJCGaeNx_5yxFSmzqi58Wi9M8Q42CmIJJ7tiOUoRvynKN4HG7hCT1xDIkFEvcNSLVdw_ug5opy0gBnDgquiKQy3bh0bckb5h4/s1600/unnamed+%252859%2529.jpg
Mbunge wa Ludewa Mhe Deogratias Haule Filikunjombe (chini) amefariki dunia katia ajali ya Chopa katika hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na rubani Kepteni William Silaa (juu kulia), mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa na ndugu yake Marehemu Filikunjombe ambao majina  hayajapatikana mara moja.

Mhe. Deo Filikunjombe, rubani na  na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya chopa namba  5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa.


Kwa mujibu wa Meya wa Ilala aliyemaliza muda wake Mhe Jerry Silaa, ambaye ni mtoto wa rubani, hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo ya Chopa. 

"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji kuwa imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha.

"Ni mepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt. William Silaa. Nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani. Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi", amesema Mhe Jerry Silaa katika kurasa zake za mitandaoni.

tangia jana habari za kuanguka kwa nchopa hiyo zilitapakaa kila kona na katika mitandao, na kuendelea hadi leo tangia asubuhi hadi baada ya ujumbe wa Jerry Silaa kupatikana mchana huu.

No comments:

Post a Comment