Maelfu ya raia wametoroka eneo hilo huku wafanyikazi wa mashirika ya utoaji misaada, wakiondolewa na kupelekwa mahali salama, baada ya mashambulio makali ya risasi kushuhudiwa kati ya waasi na wanajeshi wa serikali ya Bwana Salva Kirr.
Kutwaliwa kwa mji wa Pagak, ni pigo kubwa mno kwa waasi, ambao kiongozi wao Dkt Riek Machar, anasemekana kuwa kifungo cha nyumbani nchini Afrika Kusini.
Robo ya idadi nzima ya raia wa Sudan Kusini, wamefurushwa makwao, na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyoanza mwaka 2013, miaka miwili tu baada ya taifa hilo kujipatia uhuru kutoka nchini Sudan ya Khartoum.
No comments:
Post a Comment