Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa ya mkoa
wa Lindi inayosomwa naMkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi mara baada
ya kuwasili mkoani Lindi tayari kwa kuhudhuria kilele cha sherehe za
wakulima (Nane Nane). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Taarifa:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Lindi na
kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi.
Makamu wa Rais amewasili mkoani
Lindi tayari kwa kuhudhuria kilele cha sherehe za siku ya Wakulima
(Nane Nane) ambapo kitaifa zinaadhimishwa mkoani Lindi.
Katika Uwanja wa ndege wa kikwetu
Lindi, Makamu wa Rais pia alipokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali
pamoja na Vikundi vya ngoma ambavyo vilimlaki kwa nyimbo mbali mbali.
Kesho siku ya Kilele cha sikukuu
ya Wakulima (Nane Nane), Makamu wa Rais atapata fursa ya kutembelea
mabanda yakiwemo ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi katika maonesho hayo kwenye
viwanja vya Ngongo kisha kuhitimisha kwa kuhutubia Wananchi kwenye
maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment