Kwa mifano mbalimbali ambayo imekuwa ikituzunguka, wengi tunaamini kuwa
mafanikio ya mtu hayawezi kupatikana mpaka mtu afikishe umri fulani
lakini kuna mifano mingi ambayo inathibitisha kupata mafanikio katika
maisha haitegemei umri wa mtu.
Leo nimekutana na list ya watu 10 duniani ambao wamepata mafanikio wakiwa chini ya umri wa miaka 15.
1: Gregory Smith
Ni mmoja kati ya watu walioweza kuthibitisha mafanikio hayahusiani na
umri wa mtu baada ya kutunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel ‘Nobel Peace
Prize’ akiwa na umri wa miaka 12. Gregory alijua kusoma akiwa na umri wa
miaka miwili na kujiunga Chuo Kikuu akiwa na umri wa miaka 10. Sasa
Gregory ni kiongozi wa wanasheria duniani.
Akiwa na miaka saba, Akrit alipata umaarufu mkubwa baada ya kufanikiwa kumfanyia upasuaji rafiki yake aliyeungua moto mkononi na vidole kushikana. Alipofikisha miaka 12 alipata nafasi katika Chuo Kikuu cha India ambako alisomea udaktari na mwaka 2011 alipata nafasi ya kufanya mahojiano na mtangazaji mashuhuri wa Marekani Oprah Winfrey katika segment ya ‘Little genious’.
Cleopatra anajulikana zaidi kama mwanamuziki mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo ya MTV ambapo akiwa na umri wa miaka 3 aliweza kufanya onyesho live kwa muda wa saa 2 mfululizo mbele ya mamilioni ya mashabiki. Aliweka rekodi nyingine ya kuwa mwanamuziki mdogo kutoa album iliyofanya vizuri sokoni.
Guinness Book of Records inamtambua kwa kushika rekodi ya kuwa mtu mwenye IQ kubwa zaidi duniani kwa mwaka 1995. Akiwa na umri wa miaka minne, Kim Ung-Young alikuwa anaweza kuongea lugha za Kikorea, Kijapan, Kijerumani na Kiingereza na alipofikisha umri wa miaka 17 aliaajiriwa na Taasisi ya Mambo ya Anga ya Marekani ‘NASA’.
Mwaka 2014 Fabiano alitajwa kama Mchezaji Bora wa Chess kuwahi kutokea duniani ambapo akiwa na umri wa miaka 14 alishinda tuzo yake ya kwanza na kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kwa level ya Grandmaster.
Ni mchoraji wa picha ambaye alipata umaarufu mkubwa baada ya kuchora picha iliyouzwa kwa mamilioni ya pesa akiwa na umri wa miaka miwili. Mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka minne alifanya maonyesho katika jumba maarufu la sanaa jijini New York akiwa mchoraji pekee.
Mwaka 2008 Michael Kevin alishinda Dollar milioni 1 kwenye show iliyoitwa Who wants to be a Millionaire baada ya kujibu maswali magumu ya Sayansi na kuibuka mshindi. Kevin alianza kuongea akiwa na umri wa miezi minne na alihitimu masomo ya Chuo Kikuu akiwa na umri wa miaka 10.
Akiwa na umri miaka 6 Willie Mosconi alikuwa mchezaji mahiri wa Pool Table na aliweza kupata mafanikio mbalimbali kupitia mchezo huo na aliwahi kushinda World Straight Pool Championship kwa miaka 15 mfululizo.
Aliweka rekodi ya kuwa mtangazaji mdogo zaidi kuwahi kutokea ambapo alianzisha Show yake ya kutoa ushauri akiwa na umri wa miaka 7. Mwaka 2016 alishinda tuzo ya Mwanahabari Bora wa Kike ‘Gracie Award’. Kwa sasa Elaina Smith ni mtangazaji wa show ya asubuhi katika radio maarufu mjini Florida, Marekani.
Ni miongoni mwa watu wanaothibitisha kuwa mafanikio hayaletwi na umri ambapo akiwa na umri wa miaka minne aliweza kugundua hesabu za Algebra. Akiwa Secondary Saul Aaron Kripke alialikwa kufundisha katika Chuo Kikuu cha Harvard.
No comments:
Post a Comment