Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli anatarajiwa hapo kesho kuweka jiwe la msingi kwaajili ya Ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Juu cha Kimataifa (Standard Gauge) katika eneo la Pugu Jijijini Dar es salaam.
Kwamujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa amesema Kukamilika kwa Ujenzi huo kutarahisha shughuli za Usafiri na Usafirishaji kwa kuwa Safari ya Dar hadi Moro itatumia muda wa saa 1:16 wakati Dar hadi Dodoma itatumia muda wa saa 2:30 na safari ya Dar had Mwanza itatumia muda wa saa 7:30.
Mradi huo ambao uko chini ya Kandarasi wa kampuni za MERKEZI ya uturuki na MOTA-ENGIL AFRIKA ya ureno kwa awamu ya Kwanza utaanza na kipande chenye urefu wa KM 300 kati ya mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro kwa grahama ya dola zaidi ya bilioni moja za kimarekani.
Hata Kupitia Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam chini ya Mkuu wa mkoa Paul Makonda imesema itahakikisha vijana wengi wa kitanzania ndio wanapewa kipaumbele kwenye Ajira zitakazo zalishwa na Ujenzi huo.
No comments:
Post a Comment