Picha za satellite za uharibifu wa mafuriko nchini Peru
Uharibifu uliosababishwa na mafuriko nchini Peru tangu mwanzo wa mwaka huu.
Watu 100 wameaga na maelfu ya wengine kuachwa bila makao kutokana na
mafuriko ambayo yamekuwa yakiendelea nchini Peru tangu mwanzo wa mwaka
huu.
Barabara na madaraja yamesombwa na maji huku miji ikifurika na mashamba kugeuka kuwa mabwawa yaliyojaa matope.
Hali hii imesababisha zaidi ya miji 800 kutangaza hali ya hatari na
kuongezeka kwa bei ya chakula. Polisi wanasaidia kuleta utaratibu kwa
maeneo yaliyoathirika.
Picha hizi za sateleite zimeandaliwa na Amazon Monitoring Project (
MAAP) pamoja na makundi ya uhifadhi ya ACA na ACCA ya Peru, na
zinaonyesha jinsi maji yalivyobadilisha mazingira eneo la kaskazini
magharibi mwa nchi kati ya Januari na Mechi.
No comments:
Post a Comment