Monday, 10 April 2017

Awasha vingo'ra 150 na kutoroka Marekani

Awasha ving'ora 150 mjini Dallas Marekani na kutoroka
Mduuzi mmoja amelaumiwa kwa kufungua milio ya zaidi ya ving'ora 150 katika mji wa Dallas, huko Marekani wikendi iliyopita.
Ving'ora hivyo hutumiwa kuwaonya wakazi wakati wa hali mbaya ya anga kama vile vimbunga.
"Ving'ora vyote 156 vilianza kulia hapa mjini, jana usiku, ila tu hakukuwa na chochote," msemaji wa mji aliwaeleza wanahabari.
"Kelele iliwaamsha watu wengi sana," alisema.
Ving'ora vilianza kulia saa 11.42 usiku Ijumaa na viliendelea kwa muda wa dakika 90.
Watu wengine walirekodi video iliyokuwa na mlio huo na kuiweka kwenye mitandao .
Mafundi kutoka afisi ya usimamizi wa maswala ya dharura ilifanikiwa kuzima ving'ora na wakapata ushahidi kuwa kweli kulikauwa na mtu aliyechokora mitambo na kusababisha haya yote.
"Tunaamini kuwa aliyefanya haya yuko Dallas," taarifa kutoka kwa maafisa wa mji ilisema.
Mwaka jana mtu mmoja alidukua kompyuta zinazodhibiti taa za trafiki na kutumia ishara zake kuchapisha jumbe za utani.
Haijabainika ikiwa watu wale wale ndio waliohusika katika kisa hiki cha ving'ora.

No comments:

Post a Comment