Jina la Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda sasa hivi linatajwa
sana kwenye headlines za sakata la dawa za kulevya, hii inatokana na
kuamua kama kiongozi kuongoza vita dhidi ya dawa ya kulevya kiasi cha
kufikia hatua ya kutaja majina kadhaa ya wanaotuhumiwa.
Licha ya kuwa Paul Makonda ni kiongozi anayependa kunukuu maneno kutoka
katika kitabu takatifu cha dini yake ya kikristo Biblia, anapenda pia
kutumia nukuu za misemo ya wahenga ambayo inatumiwa na watu mbalimbali
katika harakati za kumtia moyo mtu ili kutokata tamaa katika jambo
lolote.
Asubuhi ya March 6 RC Makonda ametumia account yake ya instagram
kuandika moja kati ya nukuu zinazotumiwa na watu wengi kuhamasisha
kutokata tamaa ya jambo fulani.“Usiku hata uwe mrefu kiasi gani lazima
asubuhi itafika…Asubuhi yako iii karibu Kaza butii..you are almost
there”
No comments:
Post a Comment