Asilimia 25% ya wastaafu wa serikali nchini,wanapoteza maisha mapema
kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kushindwa kujiandaa kimaisha
mapema huku baadhi yao wakiongeza idadi ya wake na kusababisha
kuathirika kimaendeleo.
Akizungumza na watumishi wa serikali kutoka mikoa mbali mbali hapa
nchini waliobakisha muda mchache kabla ya kustaafu ,Mkurugenzi wa Chuo
cha utumishi wa umma kampasi ya Tanga,Hassanal Isaya amesema utafiti
walioufanya katika mikoa mbali mbali nchini umeonesha kuwa baadhi ya
watumishi wanashindwa kujiandaa na maisha ya kujitegemea kwa sababu ya
mazoea ya kazi.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Chuo cha utumishi wa umma nchini
Dr,Henry Mambo amesema serikali imekuwa ikitoa elimu kwa watumishi wake
ili waweze kujiandaa na maisha baada ya kustaafu hivyo amewashauri
watumishi kuacha anasa na badala yake wajikite kuwekeza katika sekta ya
elimu kwa watoto wao.
Kufuatia hatua hiyo,baadhi ya watumishi wa serikali wanaotarajiwa
kustaafu wameishukuru serikali kwa kuwakumbusha na suala la kujiandaa
baada ya kustaafu na baadhi yao wameanza mchakato wa kujitegemea ili
kuepukana na maisha ya kutangatanga katika jamii.
No comments:
Post a Comment