Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akieleza kuhusu juhudi za Serikali
katika kutengeneza mazingira mazuri ya kibiashara wakati wa mkutano na
Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord
Hollick katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick (kushoto) akifafanua jambo wakati wa Mkutano kati yake na Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani)
kuhusu nia ya kuwekeza katika ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Msalato
Dodoma, Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke, Mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa Mkutano walioongozana
na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord
Hollick, wakisikiliza kwa makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), kuhusu umuhimu wa kufanya
biashara ya bidhaa zilizoongezwa thamani ili kukuza viwanda vya ndani,
wakati wa mkutano huo jijini Dr es salaam.
Mjumbe wa Waziri Mkuu wa
Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick (kulia) akisisitiza
kuhusu kuendelea kuimalisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na
Uingereza huku Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb)
(kushoto) akimsikiliza kwa makini katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini
Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na Mjumbe wa Waziri
Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick (kulia)
baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao kuhusu Mahusiano ya kibiashara
kati ya nchi hizo mbili, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini
Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza
anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick wakiwa katika picha ya pamoja
na maafisa waandamizi kutoka nchi hizo mbili katika ukumbi wa Wizara ya
Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa Mkutano wa Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Mjumbe wa Waziri Mkuu
wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick wakisalimiana
baada ya kumalizika kwa mkutano huo na kuazimia pamoja na mambo mengine,
kufanyika kwa Mkutano utakaowakutanisha wawekezaji wakubwa wa nchi hizo
mbili, Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es
salaam.
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango ameitaka nchi ya Uingereza kutazama uwezekano wa kufanya
biashara na Tanzania kwa kununua bidhaa zilizoongezwa thamani badala ya
hali ya sasa ambapo nchi hiyo imekuwa ikinunua bidhaa ghafi ilihali
ikiingiza nchini bidhaa zake za viwandani.
Dkt. Mpango ameyasema hayo
alipokutana na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia
masuala ya Biashara Bw. Lord Hollick ailipo tembelea Makao Makuu ya
Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Amesema Tanzania inataka kuona
inauza bidhaa zake zenye thamani ambazo zitatokana na maendeleo makubwa
ya viwanda hapa nchini ikiwa ni Sera ya nchi kuwa na uchumi wa kati
unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025.
Nchi ya Uingereza imekuwa
ikifanya biashara na Tanzania kwa kiasi kikubwa na takwimu zinaonesha
nchi hiyo inaingiza bidhaa zenye thamani mara nane ya Tanzania jambo
ambalo linatakiwa kurekebishwa ili biashara iwe na manufaa kwa pande
zote mbili.
Miongoni mwa bidhaa ghafi ambazo
zimekuwa zikisafirishwa kwenda uingereza ni pamoja na Chai, kahawa na
madini ya vito huku Uingereza ikiingiza bidhaa za viwandani zenye
thamani kubwa ikijumuisha mashine (mitambo),vifaa vya umeme, bidhaa za
plastiki na madawa.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Waziri
Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw.
Lord Hollick
amebainisha nia ya nchi yake kutaka kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika
nchi za Afrika ikiwemo Tanzania baada ya Taifa hilo kuamua kujiondoa
katika Umoja wa Ulaya.
Maeneo ambayo Uingereza inapenda
kuwekeza Tanzania ni katika Sekta ya Kilimo, Nishati ya Umeme na
Usafirishaji huku kwa sasa akionesha nia ya ya nchi yake kuwekeza katika
ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato katika Makao
Makuu ya nchi – Dodoma.
Pia nchi hizo mbili zimekubaliana
kuandaa mkutano utakao wakutanisha Serikali na Sekta Binafsi ya
Tanzania kwa upande mmoja na wawekezaji wakubwa kutoka Uingereza na nchi
nyingine za Ulaya ambao utasaidia kukuza uwekezaji na biashara na
kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wa
Tanzania na nchi hizo za Ulaya ikiwemo Uingereza.
No comments:
Post a Comment