Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya
limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo
mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana
na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na
uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na
kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Kufuatia mapambano
yanayoendelea nchi nzima dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na
utumiaji wa dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya
misako na Mafanikio yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-
KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI].
Mnamo tarehe 11.02.2017 hadi
tarehe 16.02.2017 kwa nyakati tofauti, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
lilifanya misako dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji, usafirishaji na
matumizi ya dawa za kulevya. Katika misako hiyo iliyofanyika maeneo
mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya, watuhumiwa wanne walikamatwa wakiwa na dawa
za kulevya aina ya Bhangi misokoto mitatu yenye uzito wa kilogram 15 na
gram 685
- GEOFREY ADAMSON [35] Mkazi wa Mabatini
- ZUBER MWAMBENYA [24] na 3. GWAKISA ANYOSISYE [20] wote wakazi wa Mama John na
- PHILIBERT MOSES [35] Mkazi wa Nonde
- MPOKI IBRAHIM [37] Mkazi wa Kitongoji cha Igogwe Wilaya ya Rungwe
- AGUST KIHAULILO @ KIDEVU [63] Mkazi wa Igawa Wilaya ya Mbarali
- CALVINS MOHAMED [25] Mkazi wa Ilemi.
- 8. NASSORO OMARI [17] Mkazi wa Mwambene
- 9. OTHMANI SAIDI [24] Mkazi wa Mwambene
- 10. KENEDY BROWN [21] Mkazi wa mwambene
KUTEKETEZA SHAMBA KUBWA LA BHANGI
Mnamo tarehe 16.02.2017 majira ya
saa 16:20 jioni Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Kamati
Kuu ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kipolisi Mbalizi lilifanya
Oparesheni ya pamoja katika Kijiji cha Jojo kilichopo Kata ya Santilya,
Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya na
kufanikiwa kumkamata UPE NDUTA [30] Mkazi wa Jojo akiwa amelima shamba
la bhangi lenye ukubwa wa ekari moja.
Aidha katika Oparesheni hiyo zaidi
ya miche 2,000 iliyokomaa ilikutwa shambani. Pia nyumbani kwake
alikutwa na bhangi kilogram 2 na gram 145. Mtuhumiwa ni mkulima,
muuzaji/msafirishaji na mtumiaji wa dawa za kulevya [Bhangi].
KUPATIKANA NA MALI ZA WIZI.
Tarehe 15.02.2017 na 16.02.2017
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako katika maeneo mbalimbali
ya Jiji la Mbeya na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 11 waliohusika
katika kosa la kuvunja Ofisi za Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Mbeya
na kuiba kompyuta 12 ambazo zilikuwa zikitumika kufundisha.
Aidha katika msako huo vitu
mbalimbali vimekamatwa vinavyosadikiwa kuwa vya wizi pamoja na
watuhumiwa ambao kati yao wapo wanaohusika katika matukio ya uvunjaji na
ununuaji wa vitu vya wizi ambao ni:-
- GABRIEL MMASY [28] Mkazi wa Uhindini
- ITIKA KYEJO [Mwanamke] miaka 41 Mkazi wa Janibichi
- PETER MWAIPOPO [19] Mkazi wa Sinde
- WILLIAM JOSEPH [18] Mkazi wa Sinde
- RASHID SHABAN @ CHIDY [30] Mkazi wa Sinde
- FRANK CHAULA [25] Mkazi wa Sokomatola
- SALVATORY MTEGA [25] Mkazi wa Sokomatola
- KEFASY MWAMBENJA [31] Mkazi wa Kabwe
- RAPHAEL NGAILO [19] Mkazi wa Iyunga
- ABDUL RASHID [44] Mkazi wa Mbalizi
- ZAKARIA RASHID KENSE [23] Mlinzi wa Kampuni ya New Imara Security na Mkazi wa Isanga
Katika msako huo Kompyuta 11 kati ya 12 zilikuwa zimeibiwa katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Mbeya zimepatikana.
Pia katika upekuzi uliofanyika katika makazi ya watuhumiwa walipatikana na mali mbalimbali zidhaniwazo za wizi ambazo ni:-
- Kompyuta 11 na Monitor 01 aina ya HP zilizotambuliwa kuwa ni mali za Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Mbeya
- Monitor za Kompyuta 16 aina mbalimbali
- Digital Camera aina ya Canon
- Adapter 51 aina mbalimbali
- Kompyuta [Desk Top] 37 aina mbalimbali
- Laptop 10 aina ya HP, IBM, Samsung na Toshiba
- Mouse za Kompyuta 07
- Keyboard 11
- Kompyuta aina ya DELL [Working Station] 08
- Power Supply 23
- Hard Disk 64
- DVD ROM 14
- Lamp Holder 01
- Bulb World Star Lighting pcs 11
- Spika moja
- DVD Deck mbili aina ya Sony na Singsung
- Sub Woofer mbili aina ya Sea Piano na Pintech
- Stendi ya TV moja
Watuhumiwa baada ya kuhojiwa
walikiri kuhusika katika matukio ya kuvunja Ofisi Usiku na kuiba pamoja
na kununua mali mbalimbali za wizi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Naibu Kamishna wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito wa wananchi
na wakazi wa Mbeya kufika kituo kikuu cha Polisi Kati kwa ajili ya
utambuzi wa mali zao.
KUPATIKANA NA POMBE MOSHI [GONGO]
Mnamo kuanzia tarehe 01.02.2017
hadi tarehe 15.02.2017 kwa nyakati tofauti, Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya lilifanya misako katika maeneo ya Mafiati, Ilomba, Forest ya
Zamani, Itiji, Igogwe, Ngonga na Ikolo Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa
kuwakamata watuhumiwa sita wakiwa na Pombe Moshi [Gongo] yenye jumla ya
ujazo wa lita 39.
Watuhumiwa waliokamatwa wakiwa na Pombe Moshi ni:-
- FRANCIS NDEZI [32] Mkazi wa Forest
- JAMES KAJANJA [38] Mkazi wa Forest ya Zamani
- MATRIDA CHABWELA [49] Mkazi wa Igogwe
- MOSSES MWAKABENDE [51] Mkazi wa Ikolo
- MARTIN MWAMBILYA [45] Mkazi wa Ngonga Wilaya ya Kyela
- EMANUEL BROWN [21] Mkazi wa Itiji.
- GEORGE BROWN [57] Mkazi wa Itiji
- 8. ITIKA KYEJO [41] Mkazi wa Janibichi
Upelelezi unaendelea.
KUPATIKANA NA MITAMBO YA KUTENGENEZEA POMBE MOSHI [GONGO].
Tarehe 16.02.2017 majira ya saa
10:00 asubuhi Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliendelea na msako katika
maeneo ya Mtaa wa Kagera, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa
wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aliyefahamika kwa jina
la CLARENCE SUKARI [20] Mkazi wa mtaa wa Kagera akiwa na pombe haramu
ya moshi lita 53.
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa na
mitambo miwili [mapipa] ya kutengenezea pombe hiyo. Aidha Pombe hiyo
ilikutwa ikiwa imehifadhiwa katika vidumu 11 vya lita 5. Mtuhumiwa
alikiri kuwa ni mtengenezaji, muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo haramu.
KUPATIKANA NA SILAHA SHORT GUN NA RISASI ZAKE.
Mnamo tarehe 13.02.2017 majira ya
saa 18:02 jioni huko check point ya Igawa, iliyopo barabara kuu ya
Mbeya-Njombe, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya, Askari
Polisi waliokuwa doria eneo hilo walimkamata mtu mmoja aitwaye NAWAB
HUSSEN [35] Mkazi wa DSM akiwa na silaha aina ya Short gun (greener
marker) yenye namba ya usajili 26515 iliyokuwa imehifadhiwa kwenye mfuko
wa salpheti na risasi mbili ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kwenye mfuko
mweusi wa Rambo.
Askari Polisi waliokuwa doria
eneo la Check Point ya Igawa walilitilia shaka Gari lenye namba za
usajili T 289 BWQ Toyota Hiace na baada ya kufanya upekuzi ndipo
walimkuta mtuhumiwa akiwa na silaha hiyo. Mtuhumiwa alikuwa akisafiri
kwa gari hilo kutoka Mbeya kwenda DSM. Gari hilo ni mali ya Kampuni ya
KVD and Supplier LTD inayosambaza magazeti ya NIPASHE na THE GUARDIAN
mikoa ya nyanda za juu kusini. Upelelezi unaendelea.
KUKAMATA WATUHUMIWA WA UHALIFU
Mnamo tarehe 04.02.2017 hadi
16.02.2017 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya Misako/Operesheni ya
kukamata watuhumiwa wa matukio mbalimbali ya uhalifu katika maeneo ya
Ilemi, Isanga, Nonde na Airport ya Zamani – Iyela. Katika Operesheni
hiyo watuhumiwa wawili walikamatwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya
uhalifu ambao ni 1. VICTOR EBO @ TOLINGA [23] Dereva Bodaboda na 2.
ADAM PHILIMON [21] Dereva Bodaboda, Wote wakazi wa Ilemi Jijini Mbeya.
Katika upekuzi watuhumiwa hao walikutwa na vifaa mbalimbali ambavyo hutumia katika matukio ya uhalifu ambavyo ni:-
- Mizura [mask]
- Shati ya kaki yenye muonekano wa jeshi
- Panga moja
- Kapelo
- Koti
Katika mahojiano na watuhumiwa
walikiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo majalada
yake ya uchunguzi yalikuwa tayari yamefunguliwa ambayo ni UNYANG’ANYI WA
KUTUMIA SILAHA – PANGA na KUJERUHI.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Naibu Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa
wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwafichua watu na mtandao
wa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ili wakamatwe na
hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Aidha Kamanda KIDAVASHARI
anatoa wito kwa wananchi kufanya kazi na kuacha kujihusisha na biashara
haramu ya dawa za kulevya kwani inasababisha kupotea kwa nguvu kazi ya
taifa na kurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Imesainiwa na:
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment