Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema kuwa wanajeshi wanaobaka raia wanapaswa kuhukumiwa kifo.
Rais Kiir amesema hii itakuwa ni njia moja wapo ya kusafisha nchi yake na kuhakikisha uhalifu unapungua.
Haya yamesemwa wakati wa hutuba yake katika mji wa Yei kilomita 60 kutoka mji mkuu Juba.
Makundi ya haki za binadamu yaliripoti na kutuhumu kwamba wanajeshi wamekuwa wakibaka wanawake.
Matukio kama hayo hutokea mara kwa mara wakati wa vita kwani Sudan
Kusini ilikuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.
Vita hizo zilikuwa ni za kikabila na zilipelekea unyanyasaji wa kijinsia wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment