Thursday, 16 February 2017
Namna ya kuzingatia muda ili uweze kufanikiwa katika Maisha
Asilimia kubwa ya maisha ya watu duniani midomo yao hutamka ya kwamba wanataka kufanikiwa. Lakini ni idadi ndogo sana kati ya idadi kubwa ambao wanapata mafanikio hayo. Ikiwa ni pamoja ya kwamba watu wote tunaishi katika mazingira ambayo yanafanana.
Tukiangalia wote tuna masaa 24 kwa siku, wote tunatumia hewa safi ambayo hatulipii hata senti moja kwa ajili ya hewa hiyo, watu wote tunaishi katika maeneo ambayo mazingira yake yana kila aina ya rasimali ambazo kama tutaamua leo kuzitumia vyema zina uwezo wa kubadilisha maisha yetu.
Swali linakuja sasa ni wapi ambapo panatutofautisha kati ya watu wenye mafanikio na wasio na mafanikio? Ikiwa wote tunaishi mazingira ya aina moja.
Kitu kikubwa ambacho kitakusaidia kupata aina hiyo ya mafanikio au kujua ni wapi panapotutofautisha ni kujitambua. Hapa ndipo ilipo siri ya mafanikio na ambayo unatakiwa uielewe.
Kujitambua ni sehemu ambayo kila msaka mafanikio lazima aijue vyema. Kujitambua huwa na uhusiano mkubwa uliopo kati ya kitu ambacho unahitaji kukifanya. Kujua ni kile unachokitaka ndo siri ya kupata mafanikio yako.
Watu wengi kutokana na changamoto za kimaisha wamekuwa wapo tayari kufanya jambo lolote, mfano hivi hajawahi kukutana na mtu anakwambia yupo tayari kufanya jambo lolote?
Bila shaka umewahi kukutana na mtu huyo, ila ukweli ni kwamba kufanya hivi ni kuchelewa katika safari yako ya mafanikio na mafanikio. Kwani ukitaka kufanikiwa ni lazima ujue kila unachotaka kufanya kutoka nafsini mwako.
Unaweza kujiuliza maswali haya ili kuweza kujitambua na hatimaye kupata mafanikio yako.
1. Wewe ni nani?
2. Unataka kufanya nini?
3. Umetoka wapi?
4. Upo wapi?
5. Na unaelekea wapi?
Maswali hayo yote msingi wake wa mkuu ni kujiuliza lengo lako la kuja duniani ni nini?
Ukipata majibu ya maswali hayo tafadhari nakuomba uyaandike katika daftari lako na kuyachukulia hatua mathubuti, kufanya hivyo kila wakati ni hatua za kuweza kufanikiwa.
Labels:
MWANZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment