Katika bango aliloliweka katikati ya barabara Mzee Mchambua alianisha sifa tano za mke anayemtaka pamoja na namba za simu za kuwasiliana naye.
Sifa hizo ni pamoja na awe mshika dini, uvumilivu wa ndoa, uwezo wa kilimo, apendo wa mume, watoto na wajukuu pamoja na usafi wa hali ya juu.
Mzee Mchambua ambaye alizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) hivi karibuni alisema alifanya uamuzi huo baada ya kufiwa na mke wake aliyezaa naye watoto 11 na kumwacha akiwa hana mtu wa kumsaidia kutunza familia na kufanya shughuli za shambani.
Katika mazungumzo na mwandishi wa BBC, alisema tayari wamejitokeza wanawake wanne waliotaka kuolewa naye lakini hakuna hata mmoja aliyekidhi vigezo alivyoainisha.
Alisema alilazimika kutumia njia ya tangazo kwa sababu anafiri kwa umri alionao hawezi kumpata mke kwa njia ya kawaida.
Alisema endapo njia hiyo itashindikana kumpata mke mwenye sifa anazotaka atalazimika kutumia madalali kumsaidia kumtafuta mke mwenye sifa.
BBC pia ilizungumza na mmoja wa watoto wa Mzee Mchambua, ambaye alisema anaona uamuzi wa baba yake ni sawa kwa sababu ameweka sifa za mwanamke anayemtaka.
Mtoto huyo alisema wapo tayari kumpokea mke mpya wa baba yao na watamheshimu kama mama yao mzazi.
No comments:
Post a Comment