Waziri wa Mambo yaKatiba na SheriaDkt
Harrison Mwakyembe amewataka wajumbe wa Kamati ya Kimataifa
inayojishughulisha na kuzuia mauaji ya kimbari katika nchi za ukanda wa
Maziwa Makuu kuangalia upya mikakati ya kuondoa vitendo vya mauaji ya
kimbari na ukiukwaji wa haki za binadamu katika ukanda huo.
Dkt. Mwakyembe amesema Ukanda wa Maziwa
Makuu umekuwa ukishuhudia vitendo vya mauaji ya kimbari vikishamiri
licha ya kwamba kila nchi imekuwa ikichua jitihada mbalimbali na kusaini
makubaliano ya kikanda na kimataifa ya kuzuia vitendo hivyo.
Amesema wakati sasa umefika wa kujiangalia
ni kwanini vitendo hivyo vimekuwa vikishamiri pamoja na jitihada zote
ambazo kila nchi imekuwa ikizichukua ilikukomesha vitendo hivyo.
“ Ni wazi kuwa siku hizi mwelekeo wa
matukio ya kihalifu umebadilika, zimeibuka njia nyingi mpya
zinazosababisha mauaji ya kimbari na hata ukiukwaji wa haki za binadamu,
kutokana na hali hiyo kuna haja ya kuboresha mikakati yenu ili kuzuia
kuendelea kutokea kwa mauaji ya kimbari na ukiukwaji wa haki za
binadamu,” alisema.
Aidha Mhe. Waziri pia amewaambia wajumbe
wa kamati hiyo kuwa ni jukumu lao kuangalia namna ya kukabilia na
changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza na hivyo kufanya vitendo hivyo
kuendelea kuwepo miongoni mwa nchi za maziwa makuu.
Amewataka wataalamu hao kwenda mbali
zaidi na kubainisha hatua zitakazofaa kuchukuliwa za kisera, kisheria
na kiutawala ilikukabiliana nac hangamoto ya kuendelea kuwepo kwa
vitendo hivyo ili kuvikomesha ndani ya nchi za ukanda wa maziwa makuu
Mhe.Dkt Mwakyembe alikuwa akifungua
mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo na kubadilishana uzoefu wa
wajumbe wa Kamati hiyo kwa nchi za Maziwa Makuu yanayofanyika jijini Dar
es salaam. Mafunzo hayo yanajumuisha wajumbe kutoka nchi za Zambia,
Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Congo DRC, Sudani Kusini na mwenyeji
Tanzania.
No comments:
Post a Comment