Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa
ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (wapili kulia-meza kuu), akitoa
hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya Siku mbili ya kujadili jinsi ya
kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha
binadamu. Fella alisema wadau wa warsha hiyo watatoa elimu kwa umma
jinsi ya kuwasaidia idadi kubwa ya watoto ambao wameathirika. Wapili
kushoto meza kuu ni Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa
Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer.
Kushoto ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr
Qasim Sufi, na kulia ni Mratibu wa Mradi wa Shirika la Kimataifa la
Uhamiaji (IOM), Tamara Keating. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli ya
Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya
(EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland
Van de Geer akitoa hotuba yake katika Warsha ya siku mbili ya kujadili
jinsi ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya
kusafirisha binadamu nchini. Katikati ni Katibu wa Sekretarieti ya
Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella, na kulia ni Mratibu
wa Mradi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Tamara Keating.
Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es
Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa
ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (katikati), akiteta jambo na
Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika
Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer, mara baada ya Katibu
huyo kufungua Warsha ya siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na
kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu
nchini. Fella alisema baada ya warsha hiyo, washiriki hao wataanza kutoa
elimu kwa umma jinsi ya kuwasaidia idadi kubwa ya watoto ambao
wameathirika. Kushoto ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)
nchini, Dr Qasim Sufi. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt
Regency, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa
ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (wapili kulia-waliokaa),
Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika
Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer (wapili
kushoto-waliokaa), Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)
nchini, Dr Qasim Sufi (kushoto-waliokaa), Meneja wa Mradi Umoja wa Ulaya
(EU), Anna Costantini, wakiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka
Taasisi za Serikali pamoja na Mashirika yasiyokuwa ya Serikali, mara
baada ya kufunguliwa warsha ya siku mbili ya kujadili namna ya kuwalinda
na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu
nchini. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini
Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Felix Mwagara, MOHA
Serikali kwa kushirikiana na
Mashirika ya Kimataifa wameanza kujadili nyenzo mbalimbali ambazo
zitasaidia kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya
kusafirisha binadamu nchini.
Akizungumza wakati akifungua
warsha ya siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na kuwasaidia watoto
walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu, inayofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo,
Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara
Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus
Fella alisema warsha hiyo ni muhimu ikiwa na lengo la kusaidia idadi
kubwa ya watoto walioathirika nchini.
Alisema Tanzania ambayo ni kati
ya mataifa yanayoshamiri kwa biashara haramu ya kusafirisha watoto kwa
lengo la kwenda kuwatumikisha kazi katika maeneo mbalimbali nchini
pamoja na duniani kwa ujumla, kupitia nyenzo hizo zitakazo jadiliwa
zitasaidia kutoa elimu kwa umma juu ya matatizo hayo nchini.
“Nyenzo hizi za kuwasaidia na
kuwalinda wale watoto walioathirika baada ya kutoka katika maeneo
mbalimbali zitasaidia kutoa elimu ya kuwandaa kisaikolojia ili wasikate
tamaa na maisha, pia watoto watalindwa na baadaye watarudishwa kwa
wazazi wao ili waweze kuendelea majukumu mengine ya kujenga taifa,”
alisema Fella na kuongeza;
“Kumekuwepo na wimbi kubwa la
kuwasafirisha wasichana wa Kitanzania kwenda nchi za uarabuni kwa lengo
la kwenda kufanya kazi za ndani, ila wanapofika huko mambo
yanawaharibikia wanaanza kudhalilishwa, kunyanyaswa kiasi kwamba
wanashindwa kupata misaada, kutokana na manyanyaso hayo urudi nchini
wakiwa wameathirika kwa kiasi kikubwa.”
Fella alisema wadau wa warsha
hiyo watatoa elimu kwa umma kuhusu kukomeshwa kwa biashara hiyo haramu
na wazazi kutokuwaruhusu watoto wao kwenda kufanyiwa unyanyasaji huo kwa
kuwa ni kinyume cha sheria. Hata hivyo, kutokana na wimbi hilo kuzidi
kushika kasi nchini, pia wadau hao watatoa elimu ya watoto walioathirika
mara baada ya kurudi nchini ili wajitambue kutokana na mateso
mbalimbali waliokumbana nayo ili wasiweze kukata tama kutokana na
vitendo vya ukatili walivyofanyiwa katika maeneo wanayotoka.
Aidha, Mwakilishi Mkuu wa Umoja
wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi
Roeland Van de Geer alisema Tanzania ni kati ya nchi zilizoathirika na
biashara haramu ya kusafirisha watoto, hivyo elimu inahitajika ili
kukomesha biashara hii hatari.
“Watoto wa leo ni mabibi na
mabwana wa kesho, hivyo wapaswa kulindwa pamoja na kuelimishwa, Umoja wa
Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwasaidia watoto
waweze kuepuka mateso wanayoyapata,” alisema Roeland.
Warsha hiyo iliandaliwa na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya pamoja na
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na inatarajiwa kumalizika Oktoba
20 mwezi huu ambapo wadau hao wataanza kufanyia kazi nyenzo hizo
zilizojadiliwa.
No comments:
Post a Comment