Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba akiongea na Vyombo vya
Habari juu ya hatua za Serikali za kuzuia utupaji ovyo wa taka hatarishi
za Hospitalini na kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki
ifikapo Januari mosi 2017. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira
Bw. Richard Muyungi.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
TANGAZO KWA UMMA
UZUIAJI WA UTUPAJI OVYO USIO WA KITAALAMU WA TAKA ZA MAHOSPITALI.
Sheria ya usimamizi wa Mazingira
ya mwaka 2004 inapiga marufuku uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na
unaotokana na taka za mahospitali. Aidha Kanuni za Taka Hatarishi za
mwaka 2009, zinasisitiza utenganishi wa taka mbali mbali zitokazo
kwenye mahispotitali kwa kuzitibu katika namna ambayo haitaleta athari
katika mazingira na afya ya binadamu. Pia Kanuni zinahimiza matumizi ya
teknologia sahihi kama vile matumizi ya incinerators ambazo huchoma taka
za mahospitali na kuziteketeza kabisa.
Ofisi yangu imefuatilia na
kugundua kuwa taka nyingi za mahopitali, taka kutoka katika maduka ya
madawa zilizoisha muda wake zinatupwa ovyo au kuharibiwa kwa utaratibu
usio kubalika kitalaamu. Tumefuatalia na kukuta malundo ya madawa
chakavu na vifaa vya hospitali vilivyotumika katika maeneo ya visiwa
vya Bongoyo na Mbudya. Aidha madawa chakavu yanatumpwa holela katika
dampo la Pungu Kinyamwezi. Hii ni hatari sana kwa mazingira na kwa afya
ya binadamu.
Kuanzia sasa ni marufuku kutupa
taka hizi katika utaratibu usio wa kawaida. Kila hospitali na zahanati
au kituo cha afya kihahakikishe kinatumia incinerators au utaratibu
mwingine ulio sahihi kwa mujibu wa sheria ya mazingira na kanuni zake.
Aidha ninaiagiza NEMC kuanzia sasa wafanye msako mkali kubaini
mahospitali na watu wanaokiuka agizo hili. Nimewapa mwezi mmoja na
kwa wale wanaofanya hivyo waache mara moja. Kwa msako huu
atakayebainika kukiuka hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi yake.
Nichukue fursa hii kutoa tena pole kwa wezentu wa Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani kwa athari za tetemeko la ardhi.
Baada ya tatetemeko kuna athari
kubwa za kimazingira ambazo zimejitokeza. Hivyo mimi binafsi
ninafuatilia suala hili kwa ukaribu na kuhakikisha athari ambazo
zimejotokeza na zinazoendelea kujitokeza zinashughulikiwa kwa haraka.
Nimeagiza Ofisi yangu pamoja na NEMC washirikiane kwa ukaribu sana na
watendaji wa Mkoa na Kamati mbalimbali zilizoundwa kushughulikia maafa
haya na kufanya tathmini ya athari za mazingira zilizojitokeza na
kuelekeza hatua za haraka kuchukuliwa ilikupunguza madhara kwa mazingira
na binadamu.
Pia, napenda kutumia fursa hii
kuukumbusha umma juu ya dhamira ya Serikali ya kupiga marufuku
matumizi ya mifuko na vifungashio vya ya plastiki ifikapo Januari Mosi
2017.
Adhma ya Serikali ya kupiga
marufuku matumizi ya mifuko na vifungashio vya plastiki ni kuepusha
athari za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na
matumizi ya mifuko hiyo. Hivyo basi wazalishaji, waagizaji, wasambazaji,
wauzaji na watumiaji wa mifuko hiyo wanakumbushwa kuendelea na zoezi
la kuondosha pamoja na kusitisha uzalishaji wa mifuko hii.
IMETOLEWA NA
JANUARY Y. MAKAMBA (MB.)
WAZIRI WA NCHI OFISI YAMAKAMU WA RAIS
MUUNGANO NA MAZINGIRA
21/9/2016
No comments:
Post a Comment