Yemi Alade atokelezea na gauni la mil. 15
Mwanadada anayekimbiza kwenye muziki kutoka Naija, Yemi Alade hivi
karibuni katika sherehe za utoaji tuzo za Black Entertainment Television
(BET 2016) zilizofanyika nchini Marekani alitokelezea akiwa katika vazi
la gauni lenye thamani ya milioni 15.
Katika tuzo hizo ambazo Yemi alikuwa katika kipengele kimoja na mastaa
wengine wa Afrika wakiwemo Diamond, Wizkid, Black Coffee, AKA na
wengineo, Yemi alitokelezea na gauni hilo lililobuniwa na mbunifu wa
kimataifa mwenye asili ya Lebanon, Zuhair Murad.
Inasemekana kuwa si mara ya kwanza kwa mbunifu huyo kuwavalisha mastaa
mbalimbali duniani, alishawahi kuwavalisha mastaa wa muziki kama
Christina Aguilera, Kerry Washington, Cherlyl Cole na wengineo.
No comments:
Post a Comment