Wednesday, 20 July 2016

Omog aomba mechi za kirafiki kabla ya ligi kuu


 Na Chrispino Mpinge

Kocha wa Simba Mcameroon Joseph Omog ameomba kucheza michezo mitatu ya kirafiki ya kimataifa kwa ajili ya kukipima kikosi hicho.
Timu hiyo hivi sasa ipo Mkoani Morogoro kwa ajili ya kambi ya pamoja kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara chini ya Mcameroon huyo na Mganda, Jackson Mayanja.


Akiendelea kukinoa kikosi hicho Omong anaendelea na mchujo wa wachezaji wa kimataifa wanaokwenda mkoani humo kwa ajili ya majaribio.

Katibu Mkuu wa timu hiyo, Patrick Kahemele amesema yapo baadhi ya mapendekezo waliyoyapokea kutoka kwa kocha ikiwemo la kucheza mechi tatu za kirafiki kabla ya kuanza kwa ligi kuu.

Kahemele amesema, kikubwa kocha anataka kuona sehemu zenye upungufu atakazoziimarisha kabla ya kuanza kwa ligi kuu na lengo ni kuwa na kikosi imara kitakacholeta ushindani ndani ya uwanja.

Kahemele amesema, Bado hawajajua watacheza na timu gani na hivi sasa wapo kwenye mazungumzo na baadhi ya timu ambazo wasingependa kuzitaja hadi pale zitakapothibisha kucheza.

Kahemele amesema, nchi za Afrika zinatofautiana vipindi vya maandalizi ya ligi kuu, zipo nyingine ligi zao zimemalizika na nyingine ambazo zipo kwenye usajili, hivyo hali hiyo inawapa ugumu kama uongozi, lakini kila kitu watakiweka wazi hivi karibuni

No comments:

Post a Comment