Mratibu
wa Maafa Shirika la Umoja wa Mataifa la Upunguzaji Athari za Maafa
(UNISDR) Bw.Adam Fysh akielezea jambo wakati wa mafunzo ya kuandaa Kanzi
Data ya Masuala ya Athari za Maafa yaliyofanyika tarehe 19 na 20 Julai,
2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Baadhi
ya wadau wa masuala ya maafa wakifuatilia maelezo kutoka kwa Mratibu wa
Maafa Shirika la Umoja wa Mataifa la Upunguzaji Athari za Maafa
(UNISDR) Bw.Adam Fysh (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya kuandaa
Kanzi Data ya Athari za Maafa nchini yaliyofanyika kuanzia tarehe 19-20
Julai, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mratibu
wa Maafa Shirika la Umoja wa Mataifa la Upunguzaji Athari za Maafa
(UNISDR) Bw.Adam Fysh akitoa ufafanuzi kwa kikundi ‘A’ cha majadiliano
wakati wa mafunzo ya kuandaa Kanzi Data ya Athari za Maafa yaliyofanyika
katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Julai 19 na 20, 2016.
Mkurugenzi
wa Idaya ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Brig. Jenerali, Mbazi
Msuya (katikati mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa masuala ya maafa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya kuandaa
Kanzi Data ya Athari za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kulia kwake ni
Mratibu wa Maafa Shirika la Umoja wa Mataifa la Upunguzaji Athari za
Maafa (UNISDR) Bw.Adam Fysh.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Na. MWANDISHI WETU
Shirika la Umoja wa Mataifa la
Upunguzaji Athari za Maafa (UNISDR) kwa kushirikiana na Idara ya Uratibu
wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wameendesha mafunzo ya siku mbili kwa
wadau wa masuala ya maafa juu ya namna ya kutumia Kanzi Data ya takwimu
za Athari za Maafa kutoka Wizara na Taasisi za Serikali nchini.
Mafunzo hayo yalifanyika Julai 19
na 20, mwaka huu katika Ofisi ya Waziri Mkuu na kushirikisha Wizara na
Taasisi za Serikali ikiwemo; Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya
Ulinzi na Usalama wa Taifa, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Jeshi
la Zima Moto, Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Hali ya Hewa, Mamlaka ya
Usafiri wa Majini na Nchi Kavu, TAMISEMI, Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Mafunzo hayo yalijikita katika
kusaidia wadau wa masuala ya maafa katika kuongeza uwezo wa kuwa na
Takwimu sahihi za majanga yanayoikabili Nchi ya Tanzania.
Akizungumza wakati wa Mafunzo hayo
Mratibu wa Masuala ya Maafa Shirika la Umoja wa Mataifa la Upunguzaji
Athari za Maafa, Bw. Adam Fysh alieleza kuwa, Mafunzo
hayo yatasaidia kuongeza uboreshaji wa kumbukumbu za maafa nchini, “kama
ilivyokusudiwa, mafunzo yatasaidia kuwa na rekodi za kutosha,
yatasaidia ufuatiliaji, kuwa na tathimini za mara kwa mara, na
ulinganifu wa kujua nchi zingine zinafanya nini katika kukabiliaana
na athari za maafa, mafunzo haya pia yatasaidia wahusika kufanya maamuzi
sahihi na kwa wakati katika maendeleo hususani kwa kupunguza athari za
maafa hapa nchini”
Bw. Fysh aliongeza kuwa kiu yake
ni kuona nchi zinajikita katika utoaji wa taarifa zenye uhalisia na
sahihi ili kuwa na kumbukumbu na takwimu zenye kusaidia Dunia kujua
maafa yanayotokea, “Natamani kuona tunakuwa na takwimu sahihi na zenye
mpangilio zinazohusu athari za maafa hususani yanayoikabili nchi’
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Idaya ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jenerali, Mbazi
Msuya alishukuru jitihada za Shirika hilo kwa kuona umuhimu wa
kuwajengea uwezo wadau wa masuala ya Maafa na kueleza kuwa mafunzo hayo
yamekuja kwa wakati na yataleta manufaa makubwa kwa Taifa.
“Nawapongeza Shirika kwa kuona ni
vyema kuifikia Tanzania kwa kuijengea uwezo wa namna ya kuweka taarifa
muhumu za masuala ya Maafa katika kanzi data. Hii itatusaidia sana
katika kupanga mipango yetu kwa namna bora zaidi na vile vile itarahisha
katika kufuatilia kufanya tathmini”, Alisema Brig. Msuya
Naye Mtaalam wa Masuala ya Hali ya
Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa, Bi.Hellen Msemo
alieleza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kutoa fursa za kimaendeleo kwakuwa
takwimu za athari za maafa zitasaidia kuwa na mipango mizuri ya
maendeleo ya nchi na kuipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuona umuhimu
wa kuratibu mafunzo hayo.
Mafunzo ya kutumia Kanzi Data ya
takwimu za Athari za Maafa tayari yamezifikia nchi 31 duniani huku
Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi kumi na tatu za Afrika zilizonufaika
na elimu hiyo.
No comments:
Post a Comment